Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Ni ipi hukmu ya Hadiyth hii:
ذَÙ‡َـبَ الظَّÙ…َـأُ، ÙˆَابْتَÙ„َّـتِ العُـروق، ÙˆَØ«َبَـتَ الأجْـرُ Ø¥ِÙ†ْ شـاءَ اللهُ
“Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na yamethibiti malipo Allaah Akipenda”
Je, kuna du’aa yoyote iliyothibiti ya kwa ajili ya kufungulia swawm?
JIBU:
Hiyo Hadiyth si sahihi.
Mwenye kufunga du’aa yake inaitikiwa, ikiwa ataomba wakati wa kufuturu au kabla ya kufuturu.
Allaah Anasema:
ÙˆَÙ‚َالَ رَبُّÙƒُÙ…ُ ادْعُونِÙŠ Ø£َسْتَجِبْ Ù„َÙƒُÙ…ْ ۚ Ø¥ِÙ†َّ الَّذِينَ ÙŠَسْتَÙƒْبِرُونَ عَÙ†ْ عِبَادَتِÙŠ سَÙŠَدْØ®ُÙ„ُونَ جَÙ‡َÙ†َّÙ…َ دَاخِرِينَ﴿Ù¦Ù ﴾
60. Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike. [Ghaafir: 60]
Kadiri mja anavyohitaji msaada na kujikurubisha karibu na Allaah ndivyo du’aa yake inavyopokelewa.
Hadiyth uliyoitaja ni dhaifu kwa sababu (katika wapokezi kuna) Marwaan bin Saalim Al-Muqfayaa hajulikani.
[Ithaaf Al-Kiraam bi-Ajwibati Ahkaami Az-Zakaat wal-Hajj wasw-Swiyaam]
0 Comments