VYAKULA 6 VYA KUEPUKA KATIKA MWEZI WA RAMADHAAN

  • As salam aleikum warahamatullah wabarakatuh ndugu katika Iymaan zimesalia siku chache kuingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani In sha allaah, Unajua nini cha kuepuka kuhusu Ulaji wako ndani ya Ramadhani. Kuna aina 6 za chakula na ulaji ambao mfungaji anashauriwa kuepuka ili kulinda afya yake ndani ya Ramadhani, Fuatilia Makala hii upate faida.

  1. Vyakula vya kukaanga na vyakula vya mafuta mengi kama chips(french fries), Pakoras, sambusa, biryan, pilau na kadhalika. Vyakula vilivyo na mafuta mengi vina calories nyingi na virutubisho vichache hivyo kupelekea mlo usio na uwiano (imbalanced diet). Hii upelekea shibe isiyo na faida na huongeza uchovu wakati wa Ramadhani.
  2. Chumvi nyingi na vyakula vilivyo na chumvi nyingi kama Achari pickles, sauces, chips nakadhalika. Chumvi hunyonya maji mwilini, kutokana na unywaji mchache wa maji ndani ya Ramadhani, utumiaji wa chumvi nyingi unaweza kupelekea upungufu wa maji (dehydration) na udhaifu wa mwili ndani ya Ramadhani
  3. Vyakula na vinywaji vilivyo na sukari nyingi kama soda, pipi, energy drinks nk. Ingawa vinaweza kukupa nguvu ya haraka lakini Vyakula hivi vina virutubisho hafifu sana visivyo na manufaa mwilini. Pendelea juisi ya matunda.
  4. Chai na kahawa kupita kiasi wakati wa Daku. Chai na kahawa ikitumika kwa wingi ni aina ya vinywaji ambavyo huchochea kiwango kikubwa cha maji na chumvi kuchujwa kupitia njia ya mkojo(diuretics). Hii upelekea Madini, Maji na chumvi ambavyo vingehitajika mwilini wakati wa mchana kupotea kupitia njia ya mkojo.
  5. Kulala Mara tu baada ya chakula (Daku au futari) mwili unahitaji muda kumeng’enya chakula. Subiri masaa 2 baada ya kula kabla hujalala
  6. Kula kupita kiasi wakati wa Daku; Kula sana kunaweza kukuletea matatizo ya kimetabolitiki kama kushuka au kupanda sukari katika damu na kupungukiwa maji
Hayo ni mambo sita ya kuepuka, Kama una jambo la kuongezea au maoni yoyote, andika hapo chini Asante.

0 Comments