WAKATI WA KUKUBALIWA DUA KATIKA SIKU YA IJUMAA

Tunaendelea kuelezea  utukufu wa Ijumaa katika ukumbi wenu huu wa 'Nasiha ya Ijumaa', na  wiki hii tutazungumizia kuhusu 'saa katika siku ya Ijumaa ambayo dua hukubaliwa'
  

حديث أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ذَكَرَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَقَالَ: فيهِ سَاعَةٌ لاَ يُوَافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ وَهُوَ قَائمٌ يُصَلِّي، يَسْأَلُ اللهَ تَعَالَى شَيْئًا إِلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ وَأَشَارَ بِيَدِهِ يُقَلِّلُهَا       أخرجه البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayra رضى الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم  alitaja kuhusu siku ya Ijumaa na akasema: "Kuna saa (wakati) katika siku ya Ijumaa ambayo mja Muislamu hatowafikiwa nayo wakati anaswali na anamuomba Allaah سبحانه وتعالى  chochote ila Allaah Humpa"  Na Mtume صلى الله عليه وسلم akaashiria udogo wa hiyo saa (huo wakati) kwa mikono yake.   (Imetolewa na Al-Bukhari kwenye Sahihi yake) 


Bila ya shaka Muislamu atapenda kujua saa hiyo yenye kujibiwa maombi  katika siku ya Ijumaa ni ipi?  Je, ipo katika siku nzima ya Ijumaa?   Au baada ya Swalah ya Ijumaa? Au baada ya Al-'Asr?  


Ingawa siku ya   Ijumaa nzima ni siku tukufu,  kauli na  rai nyingi zimetolewa kuhusu saa hiyo, lakini kauli zilizo  sahihi kabisa ni mbili, kuwa ni aidha wakati anapokaa Imam katika minbari siku ya Ijumaa mpaka inapomalizika Swalah au baina ya Swalah ya 'Asr mpaka kuzama jua kama ilivyo katika hadithi zifuatazo sahihi.


من  حديث أبي بردة بن أبي موسى أن عبد الله بن عمر قال له أسمعت أباك يحدث عن رسول الله صلى الله عليه وسلم في شأن ساعة الجمعة شيئا ؟ قال نعم سمعته يقول سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول   }هي ما بين أن يجلس الإمام إلى أن تقضى الصلاة {
Kutoka kwa Abu Bardah bin Abi Musa kwamba inatokana na Abdullahi bin Umar kamwambia  "Umemsikia baba yako anasimulia hadithi ya Mtume صلى الله عليه وسلم kuhusu saa ya Ijumaa?  Akasema  ndio nimemsikia anasema kuwa  nimemsikia Mtume  صلى الله عليه وسلم  anasema  {(Hiyo saa) inapatikana baina ya wakati anapokaa Imaam mpaka inapomalizika Swalah}  Imetolewa na Muslim.


Riwaya nyingine ni kuwa hiyo saa iko baina ya Swalah ya 'Asr  mpaka kuzama jua na riwaya nyingine sahihi ni kuwa ni saa ya mwisho katika siku hii ya Ijumaa.   

وروى أبو داود والنسائي عن جابر عن النبي صلى الله عليه وسلم قال (يوم الجمعة اثنا عشر ساعة فيها ساعة لا يوجد مسلم يسأل الله فيها شيئا إلا أعطاه فالتمسوها آخر ساعة بعد العصر)
Kutoka kwa Abu Dawuud na An Nasaai kutoka kwa Jabir kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema {Katika siku ya Ijumaa yako masaa kumi na mbili ikiwemo saa ambayo Muislamu hamuombi Allaah  humo ila Humtakabalia, basi ishikilieni saa ya mwisho baada ya Alasiri }    


Haja ngapi tunazitaka kutoka kwa Mola wetu.  Kwa hiyo hii  ni fursa ya kuitukuza siku hii tukufu ya Ijumaa na kujitahidi kuipata hiyo saa ambayo dua zetu zitajibiwa kwa kukaa kufanya ibada zaidi katika siku hii tukufu na haswa katika hizo nyakati zilizotajwa katika hadithi hizo sahihi.

 ********

0 Comments