002-Swahiyh Fiqhis-Sunnah - Mlango Wa Twahara: Aina Za Twahara

Maulamaa wanaigawanya Twahara ya kishariy'ah katika vigawanyo viwili:
1- Twahara ya kihakika: Nayo ni Twahara ya kuondosha najisi. Hii inakuwa katika mwili, nguo na mahala.
 
2- Twahara ya kihukumu: Ni Twahara kutokana na hadathi, nayo  inahusiana na mwili. Aina hii ya Twahara ni sampuli tatu:
 
Twahara kubwa, nayo ni kuoga, Twahara ndogo, nayo ni kutawadha, na badala ya viwili hivyo vinaposhindikana, nayo ni kutayamamu.
 
KWANZA:
 
TWAHARA YA KIHAKIKA
 
Makusudio ya najisi:
Najisi  ni kinyume ya Twahara. Na najisi (kilichonajisika), ni jina la kitu chenye kuonekana kichafu kishariy'ah. Ni lazima Muislamu ajiepusha nacho na akioshe kile kilichompata katika kitu hicho.
  

0 Comments