017-Swahiyh Fiqhis-Sunnah - Mlango Wa Twahara: Nguzo Za Wudhuu

Nguzo za wudhuu ni mambo ambayo uhakika wake unajengekea kwayo kwa namna ambayo ikikosekana nguzo yoyote kati yake, basi wudhuu unabatilika na unakuwa hauzingatiwi kisheria. Nguzo hizo ni:

1- Kuosha uso wote
Uso ni sehemu ya kufanyikia makabiliano. Na mpaka wake ni kutokea kwenye mapindio ya kipaji cha uso (au tokea kwenye maoteo ya kawaida ya nywele) mpaka kwenye mashukio ya ndevu na kidevu kwa urefu, na tokea kwenye sikio hadi sikio jingine kwa upana.
Kuosha uso ni nguzo kati ya nguzo za wudhuu. Wudhuu hautosihi bila ya nguzo hii kwa neno LakeSubhana:


« يا أيها الذين آمنوا إذا قمتم إلى الصلاة فاغسلوا وجوهكم»


« Enyi mlioamini! Mnaposimama kuswali, basi osheni nyuso zenu »([1])

Kila aliyehadithia sifa ya wudhuu wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), amethibitisha kuoshwa uso. Na Maulamaa wote wamekubaliana juu ya hili.([1])Surat Al-Maaidah : 6

0 Comments