049-Swahiyh Fiqhis-Sunnah - Mlango Wa Twahara: Kutayamamu (1)

KUTAYAMAMU(*)


KUTAYAMAMU KILUGHA NA KISHARI’AH([1])

Kilugha ni kukusudia. Ikisemwa (تيممت فلانا)
Inamaanisha: Nimemkusudia fulani.

Allaah Mtukufu Anasema:
((ولا تيمموا الخبيث منه تنفقون))

((Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya..))([2])

Kishari’ah ni kuukusudia mchanga wa juu ya ardhi kwa ajili ya kuhalalika yanayohalalishwa na Wudhuu na kuoga.USHARI’AH WA KUTAYAMAMU

Kutayamamu kumethibiti katika Qur-aan, Hadiyth na Ijmaa’.

1- Katika Qur-aan ni Neno Lake Allaah Mtukufu:

((فلم تجدوا ماء فتيمموا صعيدا طيبا))

((na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lililo safi)).([3])

2- Katika Hadiyth ni neno lake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((جعلت الأرض كلها لي ولأمتي مسجدا وطهورا، فأينما أدركت رجلا من أمتي الصلاة، فعنده مسجده وعنده طهوره))

((Ardhi yote imefanywa kwangu na kwa umati wangu kuwa ni sehemu ya kuswalia na kujitwaharishia. Na popote itakapomkuta Swalah yeyote katika umma wangu, basi hapo ndipo pake pa kuswalia na pake pa kujitwaharisha)).([4])

Na Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn, amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali, kisha akamwona mtu mmoja kajitenga kando hakuswali na wengine. Akamwambia:

((يا فلان، ما منعك ألا تصلي مع القوم؟))

((Ewe fulani! Una nini usiswali na watu?)) Akajibu: “Ewe Mtume wa Allaah! Imenipata janaba na maji hakuna”. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihii wa sallam) akamwambia:

((عليك بالصعيد فإنه يكفيك))

((Tumia vumbi, kwani linakutosheleza)).
Yalipokuja maji, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimpa mtu huyu chombo cha maji akamwambia:

((اغتسل به))

((Ogea)).([5])


3- Ama Ijmaa’, Ibn Qudaamah katika “Al-Mughniy” (1/148) amesema:
“Umma wote kiujumla umejuzisha kutayamamu”.


 
(*) Katika mlango huu, nilifaidika na mengi kutokana na utafiti uliotayarishwa na kaka yangu Twaariq Saalim – Allaah Amlipe jaza Yake – kwa ajili ya kujipatia digrii ya pili katika sheria.                  
([1])“Al-Majmuu” (2/238), “Al-Mughniy” (1/148) na “Al-Mabswuut” (1/106).
([2]) Surat Al-Baqarah: 267.
([3]) Surat Al-Maaidah: 6
([4]) Hadiyth Hasan: Imetolewa na Ahmad (2/222) kupitia ‘Amr bin Shu’ayb toka kwa babaye toka kwa babuye.
([5]) Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (348) na Muslim (1535).

0 Comments