059-Swahiyh Fiqhis-Sunnah - Mlango Wa Twahara: Kutayamamu (11)

NI USO UPI WA ARDHI (MCHANGA) UNAOFAA KWA TAYAMMUMI?

Maulamaa wana rai mbili kuhusu mchanga unaofaa kutayammamia:


Rai Ya Kwanza

Ni uso wowote wa ardhi ikiwa ni changarawe, mlima, mchanga au udongo. Huu ni mwelekeo wa Abuu Haniyfah, Abuu Yuusuf na Maalik. Umekhitariwa na Shaykh wa Uislamu. Pia Ibn Hazm amelikhitari hilo, lakini yeye kashurutisha kuwa endapo kama uso wa ardhi hauna udongo, basi uwe umeshikamana na ardhi.([1])

Kati ya hoja zao ni:
1.     Ni neno Lake Allaah Mtukufu:

((صعيدا زلقا))
((Ardhi tupu))([2])
 
Na Neno Lake Subhaanahu wa Ta’alaa:

((صعيدا جرزا))
(Ardhi kame))([3])

Amesema katika “Al-Istidhkaar” (3/158): “Al-Juzur” ni ardhi ngumu isiyootesha kitu.

2.     Neno lake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا))
((...na ardhi imefanywa kwangu kuwa sehemu ya kuswalia na kitwaharisho))([4])

3.     Neno lake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((يحشر الناس يوم القيامة على صعيد واحد))
((Watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah juu ya ardhi moja)).([5])

4.     Neno lake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((جعلت الأرض كلها لي ولأمتي مسجدا وطهورا، فأينما أدركت رجلا من أمتي الصلاة فعنده مسجده وعنده طهوره))
((Ardhi yote imefanywa kwangu na umati wangu kuwa sehemu ya kuswalia na kitwaharisho, na popote itakapomkuta Swalah yeyote katika umma wangu, basi hapo ndipo sehemu yake ya kuswalia, na hapo ndipo kitwaharisho chake)).([6])

5.     Hadiyth ya Abuu Al-Juhaym kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipiga juu ya ukuta kwa mikono yake miwili, akatayammamu, kisha akamjibu mtu maamkizi.([7])

6- Ni yale yaliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba amesema:
“Uso mzuri zaidi wa ardhi ni konde na ardhi ya konde”.([8])Rai Ya Pili

Uso wa ardhi ni udongo na kinginecho hakitoshelezi.

Huu ni mwelekeo wa Ash-Shaafi’iy, Hanbali, Abuu Thawr na Ibn Al-Mundhir. Kati ya hoja zao ni:

1.   Ni ziada iliyokuja [وجعلت تربتها لي طهورا]  
[na udongo (ardhi) wake umefanywa kwangu ni twahara]([9])
katika Hadiyth ya
((جعلت لي الأرض مسجدا))

Wamesema: “Riwaya hii imehusishwa na riwaya isemayo:
((جعلت لي الأرض مسجدا وطهورا))


2.     Ni Hadiyth iliyopokelewa toka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((أعطيت ما لم يعط أحد من الأنبياء : نصرت بالرعب، وأعطيت مفاتيخ الأرض، وسميت أحمد، وجعل لي التراب طهورا، وجعلت أمتي خير الأمم)).
((Nimepewa mambo ambayo hakupewa Nabii yeyote:
Nimenusuriwa kwa kutiwa khofu maadui, nimepewa funguo za ardhi, nimeitwa Ahmad, nimefanyiwa udongo kuwa kitwaharisho, na umma wangu umefanywa umma bora zaidi)).([10])


Ninasema:
“Yenye nguvu zaidi kwangu ni kauli ya kwanza. Ni kwamba inafaa kutayammamu kwa kila kile kinachoitwa ardhi, au kila kinachobeba chochote cha ardhini kama vumbi na mfano wake”.

Ama kauli ya pili, hebu tuitazame kwa pande mbili:

Kwanza: Hakuna chochote cha kuthibitisha katika dalili zao kama ulivyoona.

Pili: Wamelichukulia neno “at-turbah” katika Hadiyth kwa maana ya udongo. Na hapa hebu tuangalie. Abuu Hurayrah katika Hadiyth iliyopo kwa Muslim anasema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinishika mkono akaniambia:

((خلق الله – عز وجل – التربة يوم السبت، وخلق فيها الجبال يوم الأحد، وخلق الشجر يوم الإثنين ..))
((Allaahu ‘Azza wa Jalla Aliumba udongo (ardhi) siku ya Jumamosi, na Akaumba humo milima siku ya Jumapili, na Akaumba miti siku ya Jumatatu…)).

Katika Kamusi ya “Lisaan Al-‘Arab”, mtunzi amesema:
"خلق الله التربة يوم السبت"
Yaani ardhi.

Ninasema: Na maana hii iko wazi katika Hadiyth, Walillaahi Al-Hamd. 
([1]) “Al-Istidhkaar” (3/157), “Al-Mabsuutw (1/108), Majmuu Al-Fataawaa” (21/364) na “Al-Muhalaa” (2/158).
([2]) Surat Al-Kahf : 40
([3]) Surat Al-Kahf : 8
([4]) Hadiyth Sahihi: Imetangulia hivi karibuni.
([5]) Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (4712) na Muslim (472).
([6]) Hadiyth Hasan: Imetangulia hivi karibuni.
([7]) Hadiyth Sahihi: Imetangulia hivi karibuni.
([8]) Isnadi yake ni dhaifu: Imetolewa na Ibn Abiy Shaybah (1/161).
([9]) Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Muslim (522), Ibn Hibaan (1697), Ad-Daar Qutniy (1/175) na Al-Bayhaqiy (1/213 – 230). Yeye amezungumzia kuhusu
([10]) Hadiyth Munkar: Imetolewa na Ahmad (1/98) na Al-Bayhaqiy (1/213).

0 Comments