12 - Wakati Wa ‘Umar Ibn Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

Maoni ya ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwa jaji Shurayh, kama ilivyotajwa hapo juu, inaeleza utaratibu wake wa kufikia maamuzi kutokana na ushahidi utakaopatikana. Sifa moja muhimu ya utaratibu wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ulikuwa, hata hivyo, ni ukweli kwamba alikutana kwa ushauri na Swahaabah na kujadiliana na masuala kwa pamoja ili kufikia kuelewa kuliko bora na kutafuta njia mnasaba ya kutoa hukumu. Kufikia kwake kwenye masuala ya kisheria, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa kama vile ni daktari mwerevu aliye makini mwenye nia ya kutoa dawa kwa ajili ya kutibu maradhi bila ya kusababisha athari mbaya.

Matokeo yake, Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ametuacha na utajiri mkubwa wa misingi ya sheria. Ibraahiym al Kakha’s (amefariki mwaka 97 Hijriyyah) alisema kwamba pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipouawa kwa ajili ya Dini: “tisa ya kumi ya elimu yote iliondoka pamoja naye.” [1]

Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema kuhusiana naye, “njia yoyote ‘Umar anayoichagua, tumeikuta ni rahisi kuifuata.” [2]

Ufahamu wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ulikuwa ni wa hali ya juu na alijaaliwa kuwa na akili timamu ya kufikiria. Hivyo, alikuwa mara moja analinganisha moja kwa mengine, na kuweza kuchunguza maeneo ya suala kurudi kwenye misingi mikuu ili kuweza kuona maana yake kwa upana. Hivi ndivyo alivokuwa kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naAbu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu), na wala hakubadilika pale alipokuwa yeye mwenyewe niKhaliyfah.

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisoma mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Ni kawaida kwake kutambua kwamba Mtume atajizuia kutokana na kuianzisha amri kwa watu kufanya jambo zuri, ijapokuwa alitaka kufanya hivyo, kwa sababu hakutaka kuwapeleka kwenye ugumu. Yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara alikuwa akisema: “Kama mimi nisingekuwa nakhofia kulazimisha magumu kwa Ummah wangu, ningeliwaamrisha kufanya jambo……fulani na fulani.” [3]

Mara nyengine atawazuia kufanya jambo fulani, na baadaye, pale atakapoona kwamba sababu ya kuwazuia haina mashaka tena, ataondosha kizuizi hichi. Katika matokeo mengine, anafikia kuzuia kitu, na watamuambia kuhusu ugumu wake, na taabu itakayopatikana kutokana na kuzuiliwa huko, hivyo atajizuia kutokana na kuzuia ili kuwalinda kutokana na magumu.

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimuona namna Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), pale anapokutana na uchaguzi baina ya vitu viwili, atachagua kile kilicho rahisi baina ya viwili; na hili lilikuwa na athari kubwa kwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu). Hakika, yeye vyema alielewa kwamba Shari’ah ina malengo na matarajio ambayo ni lazima yafahamike na kutiliwa maanani; na kwamba kuna sababu muwafaka za, na nyuma yake kama sababu za hukumu hizi; ambazo nyengine zinafanywa kwa uwazi ndani ya maandiko makuu, wakati nyengine zinatajwa juu juu tu. Aliona ni wajibu wa mwanachuoni kuchunguza sababu hizo ambazo hazikutajwa ndani ya maandiko, ili kwamba maamuzi yaweze kutumika kwenye masuala mepya na maendeleo, na kila kitu kilicholetwa chini ya uamuzi wa Allaah ili kwamba watu wasiwe na mazoea ya kutafuta kitulizo na maamuzi ya kisheria kwenye matatizo yao nje ya Sheria ya Allaah.

Hivyo, tunapoangalia mwenendo wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) katika Ijtihaad, tunakuta taratibu zilizo wazi za kufikia maamuzi, hoja zilizokuwepo nyuma yake zimeegemezwa kwa manufaa ya jamii, kwa ajili ya kuwa na hadhari ili kuzuia kufikia kutenda baya au kupinga uharibifu, na kutumia njia rahisi na ya manufaa chini ya sheria.

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwa mfano, alitangaza baadhi ya hukumu kuwa ni batili kwa sababu ya hoja za kutumika kwake kipindi kirefu haitumiki tena, au kwa sababu ya baadhi ya vipengele vya kuufuata havipo tena. Miongoni mwa hukumu hizi: maombi yake kwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba mateka wa vita vya Badr wauawe, maoni yake kuhusu Hijjah, na kwamba Mtume aliwaambia watu kwamba yeyote atakayesema: “Hapana Mola isipokuwa Allaah.” Ataingia Peponi, kwani wataegemea bila ya kufanya jitihada zaidi, maoni yake kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwamba asitoe tena mgao wa ziada kutoka kwenye hazina ya taifa kwa wale wepya walioingia kwenye Uislamu, na maamuzi yake ya kutoitumia pamoja na wengine ardhi iliotolewa.[1] Ad-Dahlaawiy, HujjatuLlaah al-Baalighah, (Misri), I, uk. 278
[2] Ad-Dahlaawiy, HujjatuLlaah al-Baalighah, (Misri), I,  uk. 278
[3] Labda Hadiyth iliyokuwa maarufu kutumika katika mtindo huu ni ile kuhusiana na kusugua meno kabla ya Swalaah (as-siwaak).

0 Comments