FAHAMU ATHARI ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA ULAJI WA CHIPS


As salaam aleikum warahmatullah wabarakatuh ndugu katika Iymaan karibu katika makala yetu hii kuhusu siha njema leo tutazungumzia hatari ya kula vibanzi (chipsi)
Kwa kiswahili fahasa hufahamika kama vibanzi lakini kwa jina maarufu ni chips. Hiki ni chakula ambacho hupendwa na watu wengi sana hasa pale unapotaka kupata chakula cha haraka na cha bei nafuu basi mawazo yako yatawaza vibanzi.
Chips au vibanzi licha ya kuwa hupikwa kwa vianzi ambavyo vina kiwango kikubwa cha sukari, lakini pia hupikwa kwa kutumia mafuta mengi na hivyo kufanya mafuta yanayoingia mwilini kusababisha matatizo mbalimbali.
Hatari kubwa ipo kwa watu wanaokula chips mara kwa mara lakini hawafanyi mazoezi kwani wanakuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo. Ukifanya mazoezi mara kwa mara yanasaidia kuyeyusha mafuta ndani ya mwili wako na hivyo kukuondoa katika hatari hiyo.
Vijana wengi sasa wanaugua magonjwa mbalimbali yanayotokana na mafuta kukusanyika kwenye miili yao ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na kutokufanya mazoezi.
Mbali na vyakula kama chipsi kusababisha magonjwa ya moyo, lakini pia hupelekea mtu kuwa mnene na kuwa na uzito mkubwa ambao mwisho wa siku husababisha magonjwa kama shinikizo la damu, magonjwa ya miguu.

0 Comments