HUKMU YA KUANZA SWALAAH YA SUNNAH (Tatwawu’) BAADA YA KUKIMIWA SWALAAH YA FARADHI NA KUIKATA SUNNAH KWAAJILI YA FARADHI

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

"Hili halijuzu, kwani imethibiti kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa maamuma anapoingia (Msikitini) na Imaam akawa kaishaanza kuswalisha, basi aingie katika safu na wala asianze kuswali Sunnah kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Itakapokimiwa Swalaah, hakuna Swalaah (inayopasa kuswaliwa) ila Swalaah ya faradhi.” [Muslim]

Lililo waajib kwa atakayeingia Msikitini na Imaam kaishaanza kusimamisha Swalaah, (ajiunge) aswali na Imaam, na aicheleweshe (hiyo Sunnah) mpaka baada ya Swalaah.
Ama kuiswali (Sunnah) huku Imaam anaswalisha basi hili halijuzu kwa Hadiyth iliyokwisha tajwa."


Na alisema tena Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) katika ukurasa wa nyuma wa kitabu hicho hicho:

“Inapokimiwa Swalaah na baadhi (ya watu) wanaswali Swalaah ya Tahiyyatul-Masjid au Sunnah (ya Raatibah [Qabliyyah/Ba’diyyah]), ilivyo kishariy’ah kwake ni kuikata (hiyo Swalaah ya Sunnah) na kujiandaa na Swalaah ya Faradhi, kutokana na kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Itakapokimiwa Swalaah, hakuna Swalaah (inayopasa kuswaliwa) ila Swalaah ya faradhi.” [Muslim]


Na akasema vilevile:

“Lakini ikiwa imekimiwa Swalaah na naye kaisharukuu rukuu ya pili, basi hakuna ubaya kuikamilisha (hiyo Swalaah ya Sunnah) kwani (hiyo) Swalaah inakuwa imemalizika; imebaki kidogo tu chini ya rakaa (kwisha).


[Al-Jaami’ fiy Fiqhi Al-‘Allaamah Ibn Baaz, uk. 295-296]

0 Comments