JINSI YA KUPIKA CHANA BATATA ZA UROJO NA CHIPSI ZA MUHOGO

Vipimo
Dengu nzima kavu - 2 Magi  (mugs
Viazi - 8-10 Vikubwa
Nyanya - 2 kubwa
Unga wa ngano / wa dengu - ¾  Magi
Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai
Ndimu - kiasi (2 vijiko vya chai)
Chumvi - kiasi
Majani ya kihindi (curry leaves) - kiasi ( majani 15)
Embe mbichi zilizokatwakatwa - 2
Rai (mustard seed) - 1 kijiko cha chai
Pilipili ya mbuzi / ya unga - kiasi
Mafuta - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Roweka dengu nzima kavu ikiwezekana usiku mzima kisha zichemshe hadi ziwive. Chuja maji yaliyobaki ziweke kavu pembeni.
  2. Chemsha viazi vilivyomenywa na kukatwakatwa vipande vikisha kuiva mwaga maji viweke pembeni.
  3. Tia mafuta kwenye sufuria tia rai, manjano na majani ya kihindi kaanga kidogo kisha tia nyanya zikaangike kidogo. Zikisha wiva kidogo tia embe mbichi ndimu pilipili na chumvi kisha wacha iwive.
  4. Tia maji kidogo halafu koroga unga na maji kisha mimina kwenye sufuria. Acha ichemke huku ukikoroga mpaka uwe kama uji.
  5. Halafu mimina dengu na viazi koroga vichanganyike onja kama ndimu na chumvi vimekolea.
  6. Epua tayari kwa kuliwa hasa na bajia,  kachori, chipsi za muhogo na chatini kama utakavyopenda.
Kidokezo:
Angalia upishi wa bajia na kachori kwenye vitafunio.

0 Comments