JINSI YA KUPIKA BOGA LA NAZI

Vipimo   

Boga la kiasi  - nusu yake
Tui zito la nazi 1 ½ gilasi
Sukari ½ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi.
  2. Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi.
  3. Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika.
  4. Epua mimina katika chombo likiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

0 Comments