JINSI YA KUPIKA KASHATA ZA KARANGA

Vipimo:
Karanga - Kilo
Sukari - 5 vikombe
Maji - 2 vikombe
Maziwa ya unga - 2 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
  1. Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.
  2. Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.
  3. Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.
  4. Paka mafuta treya  kisha mimina na utandaze upesi upesi.
  5. Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.
  6. Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.
Kidokezo:
Kama maziwa ya unga huna si lazima.

0 Comments