JINSI YA KUPIKA MAANDAZI LAINI YA KUOKA [Baked]

Vipimo 
Vikombe 3 vya unga
Kikombe 1 maziwa ya dafudafu (warm)
½ kikombe sukari
½ kikombe maziwa ya unga
Mayai 2
Kijiko 1 cha chai baking powder
½ kijiko cha hiliki ya unga
1/3 kikombe mafuta
Mchanganyiko wa hamira
2 vijiko vya kulia hamira
1 kijiko cha kulia unga
½ kikombe maji
1 kijiko cha chai sukari
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 
Weka mchanganyiko wa hamira katika bakuli dogo kisha koroga na acha uumuke kiasi dakika 5.
Kidokezo: Ukitaka hamira iumuke haraka:  Washa microwave kiasi dakika 3 bila ya kitu ndani yake. Kisha weka mchanganyiko wa hamira ndani uache uumuke basi mara moja utaumuka.

Mchanganyiko Wa Maandazi
  1. Changanya vitu vyote katika bakuli la kukandia unga la umeme kisha tia mchanganyiko wa hamira.
  2. Washa mashine ikande unga kwa mpigo wa wastani (medium speed) kwa muda wa dakika 8 takrbian mpaka donge la unga liwe laini.   
  3. Paka mafuta au unga mikononi kisha toa donge la unga ugawe madonge 9.
  4. Tandaza kila donge huku unanyunyizia unga ili usigande. Likisha tandazika likawa duara ya kiasi lisiwe nene, kata donge sehemu 4 za shape ya  pembe tatu.
  5. Pakaza mafuta katika treya na nyunyizia unga kisha panga maandazi uwache nafasi yasije kugandana yatakapoumuka.
  6. Funika kwa karatasi ya plastiki au kitambaa kusikuweko na uwazi wa kuingia hewa. Acha yaumuke muda wa saa 1 au 1 ½  kutegemea hali ya hewa.
  7. Yachome (bake) katika moto wa wastani kwa dakika 10  takriban huku unaangaza  mpaka yageuke rangi khafifu ya dhahabu.
  8. Epua yakiwa tayari panga katika sahani
 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

0 Comments