JINSI YA KUPIKA MAJIMBI (Eddoes) KWA NYAMA YA NG'OMBE

Vipimo 
Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7
Nyama ng’ombe ½ kilos
Tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha kulia
Haldi (bizari manjano/turmeric) ½ kijiko cha chai
Tui zito la nazi vikombe 2
Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Safisha nyama kisha weka chumvi, bizari ya manjano, tangawizi mbichi, ukaushe kwanza katika sufuria kwa kukaanga kaanga.
  2. Ikianza kukauka, weka maji funika uchemshe iwive.
  3. Menya majimbi ukate kate na uweke katika sufuria nyengine.
  4. Mimina supu na nyama katika majimbi uchemshe yawive majimbi.
  5. Mwisho weka tui zito la nazi uchanganye vizuri kisha weka katika moto kidogo tu bila kufunika yakiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

0 Comments