JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA MCHELE ZA NAZI NA MAZIWA

Vipimo

Tambi Za Mchele  paketi 1
Tui la nazi kikombe 1
Maziwa mazito kiasi tumia ya kopo, kikombe 1
Sukari ¾ kikombe
Samli ¼ kikombe
Zabibu kiasi
Arki (rose flavour) 1 kijiko cha chai
Hiliki ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali
  1. Chemsha tambi ziwive kiasi tu, chuja maji
  2. Katika sufuria changanya vitu vyote ukoroge katika moto kisha mimina tambi.
  3. Changanya vizuri katika moto kiasi dakika 1 tu kisha mimina katika chombo cha kupikia katika oven (Oven proof) ubanike  (bake) kwa moto wa kiasi takriban dakika 20.
  4. Epua zikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

0 Comments