JINSI YA KUPIKA UJI WA SEMBE

Vipimo   

Unga wa sembe (fine corn flour) vijiko 5 vya kulia mjazo
Maziwa ½ kikombe
Maji vikombe 2 ½ takriban
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Sukari upendavyo
chumvi ukipenda chembe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 
  1. Changanya unga wa sembe katika kibakuli pamoja na maji kiasi ukoroge.
  2. Weka maji yaliyobakia katika sufuri kisha mimina unga uliokoroga, uchemshe huku unakoroga dakika chache.
  3. Tia maziwa, sukari pilipili manga ukiwa tayari.  
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

0 Comments