JINSI YA KUPIKA VIAZI VITAMU VYA NAZI

Vipimo
Viazi vitamu - 6 Vikubwa
Tui la nazi - 3 Vikombe
Sukari - ½ Kikombe
Hiliki - 1 Kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Menya viazi vitamu na kisha vikate vipande vipande;
  2. Kosha vizuri na vitie katika sufuria na uviweke jikoni;
  3. Vikisha wiva mimina tui la nazi kisha weka sukari na hiliki;
  4. Acha tui la nazi, sukari na hiliki vichemke na vichanganyike vizuri katika viazi hivyo hadi kukauka na kubaki rojo kiasi;
  5. Pakua tayari kuliwa.

0 Comments