JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA UROJO NA DENGU (Mix)

Vipimo
Dengu nzima kavu - 2 Magi  (mugs
Viazi - 8-10 Vikubwa
Unga wa ngano / wa dengu - ¾  Magi
Bizari ya manjano - ½ kijiko cha cha
Ndimu - kiasi
Chumvi - kiasi
Pilipili ya mbuzi / ya unga - ukipenda
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Roweka dengu nzima kavu ikiwezekana usiku mzima kisha zichemshe hadi ziwive. Chuja maji yaliyobaki ziweke kavu pembeni.
  2. Chemsha maji ya kutosha na mimina unga wa ngano na bizari ya manjano kama   unavyopika uji mwepesi, koroga usigande mpaka uwive
  3. Katakata vipande vidogo vidogo vya viazi na umimine kwenye uji huo unaochemka, tia  chumvi na pilipili ukipenda.
  4. Koroga koroga visigande vikikaribia kuwiva mimina dengu zako ulizozichemsha kisha  tia ndimu ikolee mpaka viwive.
  5. Epua tayari kwa kuliwa hasa na bajia,  kachori, chipsi za muhogo na chatini kama utakavyopenda. (angalia upishi wa bajia na kachori kwenye vitafunio
Kidokezo:
Ukipenda katia vipande vya embe mbichi uchemshie badala ya ndimu.

0 Comments