JINSI YA KUPIKA WALI MWEUPE KWA MCHUZI WA KUKU WA BALTI (PAKISTANI)

Vipimo 
Kuku 1 mkate vipande vipande
Vitunguu 3  katakata  (chopped)
Nyanya 5 zikatekate  (chopped)
Tangawizi mbichi ilokunwa au ilosagwa 1 kijiko cha kulia
Thomu (kitunguu saumu) kilosagwa  kijiko  1 cha kulia
Bizari mchanganyiko (garam masala) kijiko 1 cha chai
Jira/bizari ya pilau (cummin powder) kijiko  1 cha chai
Dania/gilgilani ilosagwa (coriander powder) kijiko 1 cha chai
Mtindi/maziwa lala (yoghurt) vijiko vya kulia 4 mjazo au paketi moja ndogo.
Malai ya kupikia (cooking cream) kikombe 1
Kasuri methi (majani makavu ya uwatu/dried fenugreek leaves) 1 kijiko cha kulia
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 
  1. Osha kuku vizuri mwache achuje maji.
  2. Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu mpaka vianze kugeuka rangi ya brown hafifu. Kisha tia tangawizi na thomu ukaange.
  3. Tia kuku ukaange mpaka ageuke mweupe kisha tia nyanya endelea kukaanga ziwive.
  4. Piga mtindi vizuri katika kibakuli uwe nyororo.
  5. Epua sufuria weka kando kisha tia mtindi uchanganye vizuri pamoja na kuku.
  6. Rudisha katika moto acha uchanganyike na kuku kidogo kisha mwagia malai ya kupikia (cooking cream)
  7. Tia kasuri methi/majani makavu ya uwatu yaliyovurugwa. Acha katika moto dakika 1 tu.
  8. Epua umimine katika chombo na nyunyizia  ikiwa tayari kuliwa na wali mweupe.

Bis-swihhah wal-hanaa
 (kula kwa siha na kufurahika)

0 Comments