MLANGO WA TWAHARA : FADHILA ZA KUTAWADHA

Suala: Ni zipi fadhila za kutawadha
Jabuwabu: Zimepokelewa hadithi kadhaa kutoka kwa Bwana Mtume ﷺ katika kutaja na kuonyesha ubora na fadhila za udhu. Miongoni mwa hadithi hizo ni hizi zifuatazo:
1. Ni sababu ya kupendwa na Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu aliyetukuka Anasema:

إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}    البقرة:222}

[Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kujitwahirisha]     [Al Baqara: 222].
2. Ni alama ya umma wa Mtume Muhammad  kwa kuwa watakuja Siku ya Kiyama wakiwa weupe wa nyuso na viungo vya kutawadha
Amesema Mtume :

إِنَّ أُمَّتِي يُدْعَوْنَ يَوْمَ القِيَامَةِ غُرًّا مُحَجَّلِينَ مِنْ آثَارِ الوُضُوءِ، فَمَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمْ أَنْ يُطِيلَ غُرَّتَهُ فَلْيَفْعَلْ]     متفق عليه] 

[Hakika ya umma wangu wataitwa Siku ya Qiyama wakiwa weupe nyuso na viungo kutokana na athari ya kutawadha, basi yoyote miongoni mwenu anayeweza kurefusha weupe wake na afanye] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
3. Kunafuta dhambi na makosa
Amesema Mtume ﷺ:

مَنْ تَوَضَّأَ ، فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُجَ مِنْ تَحْتِ أَظْفَارِهِ]   رواه مسلم]

[Mwenye kutawadha akautengeza udhu wake, basi dhambi zake hutoka mwilini mwake mpaka hutoka chini ya kucha zake]  [Imepokewa na Muslim.].
4.Huinua daraja
Amesema Mtume ﷺ:

ألا أدلكم على ما يمحو الله به الخطايا ويرفع به الدرجات ؟ قالوا : بلى يا رسول الله قال : إسباغ الوضوء على المكاره وكثرة الخطا إلى المساجد وانتظار الصلاة بعد الصلاة فذلكم الرباط    رواه مسلم
[Je, nisiwajulishe nyinyi kile ambacho kwacho Mwenyezi Mungu hufuta dhambi na huinua daraja? Wakasema “Ndio, tuonyeshe” akasema: “Ni kueneza maji ya udhu kwenye viungo, na kukithirisha hatua za kwenga misikitini na kungojea Swala baada ya Swala. Hiyo ndiyo jihadi]  [Imepokewa na Muslim.]

0 Comments