MLANGO WA TWAHARA : MAANA YA TWAHARA

Maana ya Twahara

Suali: Ni nini Maana ya Twahara ki Lugha na Kisheria ?
Jawabu: Utwahara kilugha
Kujisafisha na kujitakasa na uchafu
Utwahara kisheria
Utwahara kutokana na hadathi -Kujitwahirisha na najisi
VIGAWANYO VYA TWAHARA

Suali: Twahara inagawanyika sehemu ngapi?
Jawabu: Twahara inagawanyika sehemu mbili:

1. Utwahara wa ndani
Nao ni kuusafisha moyo na ushirikina na maasia na kila chenye kuutia doa. Haiwezekani kuhakikishika utwahara iwapo kutakuwa na uchafu wa ushirikina ndani ya moyo, kama ilivyo katika maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ   التوبة:28
 [Enyi Mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, basi na wasiukaribie Msikiti wa Haram (Msikiti wa Makka) baada ya mwaka wao huu. Na mkiwa mnaogopa umasikini, basi Mwenyezi Mungu Atawakwasisha nyinyi kwa fadhla Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi Mwenye hekima} [8: 28]
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu  alisema:
المؤمن لا ينجس.]    رواه البخاري]
[Muumini hanajisiki.] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim]
2.Utwahara wa Nje
Nao ni utwahara wa mwili kutokana na hadathi na najisi.
Na inagawanyika vigawanyiko viwili:
1.Utwahara kutokana na hadathi (hali ya kutokuwa na udhu na kuwa na janaba)
Hadathi ni kile kinachotukia katika mwili kikamzuia Muislamu kufanya ibada ambazo zinahitaji utwahara, kama kuswali, kutufu kwenye Alkaba na zinginezo. Na inagawanyika vigawanyo viwili:
2. Kujitwahirisha na Najisi:
Nao ni kuiyondoa najisi mwilini na nguoni na sehemu ya kufanya ibada, Na kuondoa najisi ni lazima kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliye tukuka:
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ}     المدثر:4}
"Na nguo zako zitwahirishe"   [74: 4]
Na neno lake Mtume ﷺ:
قوله صلى الله عليه وسلم : إذا جاء أحدكم إلى المسجد فلينظر فإن رأى في نعليه قذرا أو أذى فليمسحه وليصل فيهما . رواه أبو داود
[Mmoja wenu akija msikitini na atazame, akiona uchafu au kitu cha kuudhi kwenye viatu vyake basi na avipanguse kisha aswali navyo].  imepokewa na Abuu Daud.

fungua kiungo hiki ili kusoma darsa inayofuata Vigawanyo vya maji

0 Comments