MLANGO WA SWALA : FADHLA ZA SWALA

Suali: Ni zipi Fadhla za Swala?
Jawabu: Swala ina Fadhla nyingi Miongoni mwa fadhla zake ni hizi:
1. Swala ni nuru kwa mwenye kuswali. Mtume ﷺ amesema:

 والصلاة نور]       رواه مسلم] 

[Na Swala ni Nuru]       [ Imepokewa na Muslim.].

2. Swala ni kafara ya dhambi. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema:

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ}       هود:114}

"Na simamisha Swala ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zinazokaribiana na mchana. Hakika mema yanafuta maovu. Hayo ni makumbusho kwa wenye kukumbuka"      [11: 114].

Na amesema Mtume ﷺ:

رَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ، هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ؟  ، قَالُوا: لَا يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ، قَالَ:  فَذَلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، يَمْحُو اللهُ بِهِنَّ الْخَطَايَا      رواه البخاري ومسلم
[Mnaonaje, lau kuna mto mlangoni mwa mmoja wenu ambao anaoga ndani yake kila siku mara tano, je kutasalia chochote cha uchafu mwilini mwakeWakasema: Hakutasalia uchafu wowote katika mwili wake. Akasema Mtume ﷺ: Huo ndio mfano wa Swala tano,. Mwenyezi Mungu kwa hizo Swala anayafuta madhambi]  [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Swala ni sababu ya mtu kuingia Peponi. Mtume  alimwambia Rabi’ah bin Ka’ab, alipomtaka wasuhubiane naye Peponi,: Mtume akamjibu:

[ فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ ، بِكَثْرَةِ السُّجُودِ ] 

[Nisaidie kwa kuishughulisha nafsi yako kwa kusujudu sana]     [Imepokewa na Muslim.].

0 Comments