MLANGO WA TWAHARA : SUNNA ZA KIMAUMBILE

SualiNi nini Maana ya  Sunna za maumbile?
JawabuSunna za kimaumbile Mambo mazuri ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia watu nayo, ni ambayo yanamfanya mtu akamilike mpaka afikie daraja ya sifa bora na pambo zuri.
Imepokewa kutoka kwa Aishah radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume ﷺ amesema:

عشر من الفطرة: قص الشارب وإعفاء اللحية، والسواك، واستنشاق الماء، وقص الأظافر، وغسل البراجم، ونتف الإبط، وحلق العانة، وانتقاص الماء، يعني الاستنجاء" قال الراوي: ونسيت العاشرة إلى أن تكون المضمضة     رواه مسلم

[Mambo kumi ni katika sifa za kimaumbile: kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kupuliza maji, kukata kucha, kusafisha makunjo viungoni, kusumua nywele za makapwa kunyoa nywele sehemu za siri, na kutamba kwa maji na kusukutua]     [Imepokewa na Muslim.].

1.Kupiga mswaki
Mswaki ni kipande cha mti wa mpilipili – au mfano wake- kinachotumiwa kusafisha meno na chakula kilichogandamana na kuondosha harufu mbaya
Na Kupiga mswaki kumesuniwa nyakati zote, kwa kauli ya Mtume :

السواك مطهرة للفم، مرضاة للرب ]  رواه النسائي وإبن ماجة]

[Kupiga mswaki kunatwahirisha kinywa, kunamridhisha Mola]   [Imepokewa na Annasaai na Ibnu Maajah ].

FAIDA YA MSUWAKI
Miongoni mwa faida za mswaki ni kuwa unasafisha kinywa duniani, na unamridhi Mwenyezi Mungu akhera. Nao unatia nguvu meno, unayashikanisha masinye, unatakasa sauti na unamchangamsha mja.
2.Kusukutua na kupuliza maji puani
Ni Kutia maji kinyawani na kuyatikisa kisha kuyatema,na Kupaliza puani kuyavuta maji puani kwa pumzi kisha kuyatoa
 3. Kutamba
Kutamba ni kuondoa athari ya kilichotoka kwenye tupu ya mbele au ya nyuma kwa maji yenye kutwahirisha.
 4. Kupunguza masharubu na kuyafanya madogo
Makusudio ni kuyapunguza sana, kwa kufanya hivyo kunapatikana uzuri na usafi na kuenda kinyume na makafiri.
 5. Kufuga ndevu
Nako ni kuziacha na kutozigusa
Ni haramu kunyoa ndevu, kwa amri iliyokuja ya kuzifuga na kuziacha amesema Mtume ﷺ :

جزوا الشوارب وأرخوا اللحى خالفوا المجوس ]    رواه مسلم]

[Kateni masharubu na fugeni ndevu, wakhalifuni Majusi]    [Imepokewa na Muslim.].

6.Kunyoa nywele sehemu za siri.

FAIDA
Imethubutu kielimu kwamba kunyoa sehemu hizo kunatunza afya ya mwili, nguvu zake na usalama wake, kwa kuwa kule kuwa na nywele nyingi sehemu hii kunasababisha vijipu kwenye ngozi ambazo hudhuru mwili.
7. Kutahiri na kupasha tohara
Kumtahiri mwanamume,
Ni kuondoa kigozi kinachofunika kichwa cha dhakari kwa mwanamume.
Kumpasha tohara mwanamke
Ni kukata kinyama kilichozidi kilichoko juu ya sehemu ya kuingiza dhakari ya mwanamume.
 Kutahiri ni kwa mwanamume, na kupasha tohara ni kwa mwanamke kwa kuwa mtume ﷺ alimwambia Ummu Atiyyah radhi za Allah ziwe juu yake nayeye alikuwa akipasha twahara wasichana:

لا تُنْهِكِي فَإِنَّ ذَلِكَ أَحْظَى لِلْمَرْأَةِ وَأَحَبُّ إِلَى الْبَعْلِ]      رواه أبوداود والطبراني] 

[Kata kidogo wala usifeke, kwani kufanya hivyo kunakufanya hapo mahali pawe na maangalizi mazuri na kunamfurahisha mume].  [ Imepokewa na Abuu Daud na Al Twabraniy na kusahihishwa na Al Baniy katika Sunan ya Abii Daud].
MAELEZO
Kutahiri ni lazima kwa wanaume, ni sunna kwa wanawake.
Na hekima ya mwanamume kutahiriwa ni kuitwahirisha dhakari na najisi iliyopo kwenye kigozi kinachofunika kichwa cha dhakari. Ama kwa mwanamke ni kule kung’ara kwa uso wake,na kuziweka sawa Shahwa zake.
8. Kukata kucha
Nako ni kuzikata ili zisiwe ndefu
 9. Kusumua nywele za makapwa
Yaani Kuondoa nywele zinazoota makapwani, kwa kuwa kuziondoa ni katika usafi na kuondoa harufu mbaya zinazokusanyika kwa kuwako nywele hizi.
10. Kuosha makunjo kwenye viungo
Baadhi ya wanavyuoni wameyaweka pamoja hayo makunjo na uchafu unaokusanyika masikioni na shingoni na baadhi ya sehemu za mwili.

MDA ULIOWEKWA NA SHERIA
Ni karaha kwa mtu kuacha kucha, pia nywele za makapwa, nywele sehemu za siri na masharubu zaidi ya siku arubaini. Imepokewa na Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake asema:

وقت لنا رسول الله صلى الله عليه وسلم في قص الشارب، وقلم الظفر، ونتف الإبط، وحلق العانة، أن لا نترك شيئاً من ذلك أكثر من أربعين ليلة     رواه مسلم
[Mtume wa Mwenyezi Mungu  alituwekea wakati wa kupunguza masharubu, kukata kucha, kunyoanywele sehemu za siri na kusumua nywele za makapwa kuwa visiachwe zaidi ya siku arubaini]
[Imepokewa na Muslim.].

0 Comments