ANAWEKA PESA KATIKA SAVING ACCOUNT, ANAWEZA KUZITUMIA KWAAJILI YA HIJJAH?

SWALI:

ASSALAAMU ALEYKUM WARAHMATUL LLAAHI WABARAKAATUH
Sheikh mimi nina wazazi wangu wawili 60 & 64yrs, toka nilipokuwa Africa nilikuwa na nia ya kuwapeleka mecca ili wakahijji. Lakini ilikuwa hali si hali! Hivi sasa alhamdulillahi nimefika America nilipata kazi nikajaribu kufungua free saving account isiokua na riba interest wala ukwaju, ni just exactly nilichokitia, hiyo ndio itakayokuwa nauli yao, sasa hivi mambo tena yashaiva nimejikamilisha, nakutana na walee MINAL JINNATI WANNAAS washaanza kunitia wasiwasi. Yaani wasema kuwa pesa za hawa wazungu wao huchukua interest au riba kwenye benki ndio mshahara wanaotupa, sasa hawa mashekhe bandia wasema haifai kuendea hijja au kufanyia mema hizo pesa na ilhali mimi nilifanyia kazi halali wala sikuhitaji interest yao!
So sheikh nini kuhusu hayo, je yafaa? Je na mimi ujira wangu ni upi?
WABILLAHI TAWFIIQ (mungu awafanyie wepesi katika kuyahandle haya maswali mengi yasiyoisha.......amiin)


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuweka pesa zako katika saving account.

Hakika ni kuwa chumo la halali unalopata kwa kufanya kazi ya halali ni miongoni mwa Ibadah ambayo inalipwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mwenyewe.
Hivyo, unapofanya kazi ya halali unayolipwa mshahara wako ni halali yako. Unapoutimia katika kheri unapata thawabu na ukiutumia katika maovu unapata madhambi. Mas-alah ya kuweka pesa benki hizi ambazo ni za Ribaa ni jambo ambalo lina utata isipokuwa kama kuna dharura ambayo imebidi kuwa katika hali hiyo. Bila shaka kukiwa na benki ya Kiislamu inakuwa ni vyema na bora kwako kuweka akiba yako hiyo katika benki hiyo.
Maadamu pesa zako unazoziweka katika akiba haziongezeki basi akiba yako hiyo ni halali kabisa. Unafaa uzitumie katika kheri, na kuwapeleka wazazi wako Hija ni miongoni mwa 'amali njema sana. Tumia pesa zako hizo katika kheri hiyo ya kuwasaidia wazazi wako au kuzitumia katika ‘amali nyingine nzuri yoyote hakuna ubaya bali utakuwa unapata thawabu. Na ikiwa wewe hukufanya Hijjah, ni bora uharakishe nawe kuifanya.

Na Allaah Anajua zaidi

0 Comments