IMAAM IBN 'UTHAYMIYN: KUEPUKANA NA RAFIKI WAOVU NA KUANDAMANA NA RAFIKI WEMA

Kuepukana Na Rafiki Waovu Na Kuandamana Na Rafiki Wema

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

Inampasa mwana Aadam mwenye akili atafakari kuhusu rafiki zake. Je, wao ni rafiki waovu?  Basi ajiweke mbali nao kwa sababu wao ni maadui wakubwa zaidi kuliko ugonjwa wa ngozi wenye kuambukiza.

Au je, wao ni marafiki wa khayr? (Ikiwa) Wanamuamrisha yeye mema na wanamkataza munkari na wanamfungulia milango ya khayr? Basi ashikamane nao.


[Majumuw’ Al-Fataawaa (9/351)]

0 Comments