UKUMBUSHO WA SWAWM YA 'ARAFAH 9 Dhul-Hijjah 1438H (Alkhamiys 31 Agosti 2017 M)

Tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kufunga Swawm siku ya 'Arafah. Fadhila yake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili kwa dalili ifuatayo:  


 عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْيُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم
 Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]

تَقَبَّلَ اللهُ مِنَّا وَمِنْكُمْ

Allaah Atutakabalie Sisi Na Nyinyi

'Arafah 9 Dhul-Hijjah itakuwa ni Alkhamiys tarehe 31 Agosti 2017M. 'Iydul-Adhwhaa 10 Dhul-Hijjah itakuwa Ijumaa tarehe 1 Septemba 2017M.


Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayetaka KuchinjaTunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa (anayewakilisha mtu kumchinjia), kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele za mwili na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:  

عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ )) وفي رواية: ((فَلا يَمَسَّ مِنْ شَعَرِهِ وَبَشَرِهِ شَيْئًا))
Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)) na katika riwaaya nyengine ya Muslim (1977); ((basi asitoe kitu katika nywele zake wala ngozi yake)) [Muslim]

Ukumbusho Wa Takbiyrah Katika Masiku Kumi Na Tatu Ya Dhul-Hijjah:
Kadhalika tusisahau kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyrah  kuanzia unapoandama mwezi wa dhul-Hijjah mpaka mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake.
Inavyopasa kufanya Takbiyrah:
   اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ،  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd
Bonyeza upate takbiyrah kwa sauti:


Inapasa kuwakumbusha ndugu wengine mafunzo haya na kuwasisitiza ili kila mmoja apate thawabu za kufufua Sunnah hizi ambazo wengi wamegafilika nazo.
Thawabu hizo zitazidi kuongezeka kwa yule atakayeanza kumfundisha mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kufundishwa: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ .
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Atakayetenda kitendo kizuri (Sunnatun-Hasanah) katika Uislaam kisha nacho kikafuatwa kutendwa, ataandikiwa mfano wa ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao.”  [Muslim]

0 Comments