005-Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Du’aa Makhsusi Ya Laylatul-Qadr- Kuomba Al-'Afw (Msamaha)

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Du’aa Khasa Ya Laylatul-Qadr Kuomba Al-'Afw (Msamaha)


 اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي
Allaahumma Innaka ‘Afuwwun Tuhibbul-‘afwa fa’fu ‘anniy

Ee Allaah, hakika Wewe Mwingi wa kusamehe Unapenda kusamehe basi nisamehe.
[At-Tirmidhiy, Ahmad, Ibn Maajah, na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/170)]

Pia kumwita Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Majina Yake Mazuri Yanayohusiana na kuomba msamaha na maghfirah. Unamwita Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Majina hayo kwa wingi bila ya kuwekea idadi maalumu au kuambatanisha na kitendo maalumu.

يــــــَــــاعَفُـــــــــــــوُّ   يَاغَفـــُــــــورُ
Yaa ‘Afuwwu Yaa Ghafuwru.
Ee Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.

0 Comments