014-Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Kuhesabiwa Hesabu Nyepesi Siku Ya Qiyaamah

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kuomba Kuhesabiwa Hesabu Nyepesi Siku Ya Qiyaamahاللَّهُمَّ حَاسِبْنِي حِسَابًا يَسِيرًا
Allaahumma haasibniy hisaaban -yasiyraa

Ee Allaah nihesabie hisabu iliyo nyepesi  

Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) alimuuliza Rasuli wa Allaah (سبحانه وتعالى) alipomaliza kuisoma du’aa katika Swalaah: “Ipi hesabu iliyo nyepesi?” Akasema: ((Kwamba [Allaah] Atatazama kitabu chake [kilichorekodiwa ‘amali] kisha Amsamehe kwani hakika mwenye kuhojiwa hesabu siku hiyo ee ‘Aaishah ameangamia, na kila kinachomsibu Muumini Allaah عز وجل  Humfutia ([dhambi] japo ikiwa ni mwiba umchomao)) [Imaam Ahmad]


0 Comments