039-Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Du'aa Ambayo Ni Hazina Kuliko Hazina Ya Dhahabu Na Fedha!

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Du'aa Ambayo Ni Hazina Kuliko Hazina Ya Dhahabu Na Fedha! اللَّهُمَّ إِنَّي أَسْألُكَ الثَّباتَ فِي الأَمْرِ، والْعَزِيمَةَ عَلى الرُّشْدِ، وَأسْألُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، وأسْألُكَ شُكْرِ نِعْمَتِكَ ، وحُسْنَ عِبَادَتِكَ، وأسْألُكَ قَلْبًا سَلِيمًا، ولِسَانًا صَادِقًا، وأسْألُكَ مِنْ خَيْرِ ما تَعْلَمُ، وأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا تَعْلَمُ، وأسْتَغْفِرُكَ لِمَا تَعْلَمُ، إنَّكَ أنْتَ عَلاَمُ الغُيُوب

Allaahumma inniy as-alukath-thabaat fil-amri, wal-‘aziymata ‘alar-rushdi, wa as-aluka muwjibaati Rahmatika, wa ‘azaaima maghfiratika, wa as-aluka shukri ni’matika, wa husna ‘ibaadatika, wa as-aluka qalban saliyman, wa lisaanan swaadiqan, wa as-aluka min-khayri maa Ta’lamu wa a’uwdhu bika min sharri maa Ta’lamu, wa astaghfiruka limaa Ta’lamu innaka Anta ‘Allaamul-ghuyuwbi

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kuthibitika katika jambo (Dini na utiifu), na  azimio juu ya uongofu, na nakuomba haki yenye kuwajibisha Rahmah Zako, na azimio  la maghfirah Yako, na nakuomba kushukuru neema Zako, na uzuri wa kukuabudu, na nakuomba moyo uliosalimika, na ulimi usemao kweli, na nakuomba kheri Unazozijua na najikinga Kwako shari Unazozijua, na nakuomba maghfirah kwa Unayoyajua, hakika Wewe ni Mjuzi mno wa ya ghaibu.

Imepokelewa kutoka Shaddaad bin Aws (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ee Shaddaad bin Aws, ukiona watu wanaweka hazina dhahabu na fedha, basi zidisha maneno haya)) [Atw-Twabaraaniy, Taz. As-Silsilatusw-Swahiyhah (3228]

Faida:  Moyo uliosalimika ni moyo uliosalimika na kufru, shirki, riyaa, bid’ah, unafiki, maovu, husda, chuki na kila ovu.

0 Comments