058-Du'aa Za Nabiy (Swalla-Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallaam): Kinga Ya Kuangamia, Kuzama, Kuungua, Kughilibiwa Na Shaytwaan Wakati Wa .....

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kinga Ya Kuangamia, Kuvunjika, Kuzama, Kuungua Moto, Kughilibiwa Na Shaytwaan Wakati Wa Mauti...


  
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ التَّرَدِّي ، وَالْهَدْمِ ، وَالْغَرَقِ ، وَالْحَرَقِ ،  وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ يَتَخَبَّطَنِي الشَّيْطَانُ عِنْدَ الْمَوْتِ ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ فِي سَبِيلِكَ مُدْبِرًا ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ لَدِيغًا

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minat-taraddiy, wal-hadmi, wal-gharaqi, wal-haraqi, wa a’uwdhu bika an yatakhabbatwniyash-shaytwaanu ‘indal-mawti, wa a’uwdhu bika an amuwta fiy sabiylika mudbiraa, wa a’uwdhu bika an amuwta ladiyghaa

Ee Allaah, hakika  mimi najikinga Kwako kuangamia na kuvunjika na kufa kwa kuzama na kuungua na Moto, na najikinga Kwako kughilibiwa na shaytwaan wakati wa mauti, na najikinga Kwako kufa  nikiwa  mwenye  kugeuka nyuma katika njia Yako [kukimbia vita] na najikinga Kwako kufa kwa kun’gatwa [na mdudu wa sumu]


[Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy  -  Swahiyh An-Nasaaiy (3/1123)]

0 Comments