074-Du'aa Za Nabiy (Swalla-Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallaam): Kuomba Qur-aan Kuwa Ni Uhuisho Wa Moyo Na Nuru, Kuondokewa Huzuni,Wahka

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kuomba Qur-aan Kuwa Ni Uhuisho Wa Moyo Na Na Nuru,
Ufumbuzi Wa Huzuni Na Kuondokewa Wahka  
 اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ، وَابْنُ عَبْدِكَ، وَابْنُ أَمَتِكَ، نَاصِيَتِي بِيَدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ، أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ، أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي، وَنُورَ صَدْرِي، وَجَلَاءَ حُزْنِي، وَذَهَابَ هَمِّي

Allaahumma inniy ‘abduka, ibnu-‘abdika, ibnu-amatika, naaswiyatiy Biyadika, maadhwin fiyya hukmuka, ‘adlun fiyya qadhwaauka, as-aluka bikullismin huwa Laka, sammayta bihi Nafsaka aw Anzaltahu fiy Kitaabika, aw ‘Allamtahu ahadan min Khalqika, awis-staa-tharta bihi fiy ‘ilmil-ghaybi  ‘In-daka, an Taj-’alal-Qur-aana rabiy’a qalbiy, wanuwra swadriy, wajalaa-a huzniy, wa dhahaaba hammiy.

Ee Allaah hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Chako, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita  Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako, nakuomba Ujaalie Qur-aan kuwa ni rabiy' (uhuisho, raha, furaha na ustawisho) wa moyo wangu na nuru ya kifua changu, na ufumbuzi wa  huzuni yangu, na sababu ya kuondoka wahka wangu.


[Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayefikiwa na dhiki na huzuni kisha akasema  (Du’aa hiyo) hakuna isipokuwa Allaah Atamuondoshea dhiki na huzuni na Atambadilisha badala yake faraja.” Ikasemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Je tujifunze? Akasema: ”Ndio, inampasa kwa mwenye kuisikia kujifunza.” [Ameipokea Ahmad (1/391) [452], Al-Haakim (1/509) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah(199) na Al-Kalimi Atw-Twayyib (124)]0 Comments