Vipimo
Maharage - 3 Vikombe
Tui la nazi zito - 1½ kikombe
Kitunguu - 1 kikubwa
Nyanya - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 3
Chumvi - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka maharage, kasha chemsha maharage hadi yawive haswa yalainike
- Katakata kitunguu, nyanya, na thomu kisha miminia katika maharage
- Tia tui la nazi na subiri kidogo lichemkie humo
- Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi na kisha funika kwa muda kadhaa hadi libaki rojo rojo
- Baada ya hapo pakua na tayari kuliwa
Post a Comment