September 25, 2017

JINSI YA KUPIKA NYAMA YA KICHINA YA KUKAANGA NA MBOGA (Chinese Fried Beef)

Vipimo
Nyama  (Beef Pasande)  - 1 LB
(Isiyo na mafupa iliyokatwa
vipande vyembamba vya duara)
Kitunguu saumu(thomu) na Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Sosi ya Soya (soy sauce)  - 2 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Karoti  - 1
Maharage ya kijani (spring beans)  - 1 kikombe
Pilipili mboga kijani - 1
Kabeji -  2 vikombe
Vitunguu vya kijani  - 2 miche
Mafuta - ½ kikombe 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1)    Katakata nyama vipande virefu vidogo vidogo.
2)    Roweka Nyama kwa chumvi, thomu na tangawizi, pilipili manga, sosi ya soya kwa muda kama saa.
3)    Katakata karoti vipande virefu virefu vidogo kiasi.
4)    Katakata pilipili mboga
5)    Kata Kabeji nyembamba kiasi.
6)    Weka mafuta katika karai kaanga nyama mpaka iwive.
       (Karai nzuri kutumia ni ya kichina inayoitwa 'wok' lakini sio lazima)
7)    Weka karoti na maharage ya kijani (spring beans) endelea kukaanga kwa dakika chache tu.
8)    Usiwache mboga zikawiva sana. 
9)    Tia kabeji na pilipili mboga na ukaange kwa dakika moja tu.
10)  Katia vitunguu vya kijani.
11)  Epua na tayari kuliwa. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only