KAULI YA SWAHABA KUHUSU BAADHI YA AAYAH KATIKA QUR-AAN

Aayah zinazotaja majuto ya nafsi pale inapotolewa roho kwa sababu ya  maovu iliyoyatenda zilizomo katika Surat Az-Zumar, zimetangulizwa na Aayah  ambao yenye kutia matumaini makubwa baada ya mwanaadam kutenda madhambi, nayo ni

((قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ))
((Sema: Enyi waja Wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na Rehma ya Allaah. Hakika Allaah Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kughufuria, Mwenye Kurehemu))  [Az-Zumar: 53] 

Imetoka kwa Sunayd bin Shakal ambaye kasema kwamba; Nimemsikia Ibn Ma'suud رضي الله عنه  akisema;   
 Aayah tukufu kabisa katika kitabu cha Allaah سبحانه وتعالى  ni

(( اللّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوم))   
Allaah - hapana ilaah [mungu] apasaye kuabudiwa kwa haki ila Yeye Aliye Hai daima,  Msimamia mambo yote milele daima))  [Al-Baqarah: 255]

Aayah iliyokuwa na ufafanuzi kabisa kuhusu mazuri na maovu ni;
(( إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ ))
((Hakika Allaah Anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani)) [An-Nahl:90]

Aayah yenye kuonyesha matumaini makubwa kabisa ni:

((قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ))
((Sema: Enyi waja Wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na Rehma ya Allaah. Hakika Allaah Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kughufuria, MWenye Kurehemu))  [Az-Zumar: 53] 

Aayah iliyokuwa ni dhahiri kabisa katika kumtegemea Allaah سبحانه وتعالى ni:

 ((وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا)) ((وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ))

((Na anaye mcha Allaah Humtengezea njia ya kutokea)) ((Na Humruzuku kwa jiha asiyo tazamia)) [At-Twalaaq: 2-3]

Masruuq akamwambia (Sunayd bin Shakal); Umesema kweli (kwamba kauli hiyo kasema Ibn Mas'uud رضي الله عنه ) [At-Twabaraniy 9:142]

0 Comments