JINSI YA KUPIKA KHUBZ RAQAAIQ MIKATE MEPESI MIKAVU

Vipimo Aina ya 1
Unga wa shayiri (Barley) - 3 vikombe
Unga wa atta namba 2 au 3 -  2 vikombe
Maji - kiasi
Chumvi - kiasi 
Vipimi Aina ya 2  
Unga wa atta no. 2 au 3 -  4 vikombe
Maji -  2 ½ takriban
Chumvi -  kiasi 
Vipimo Aina ya 3
Unga wa shayiri au atta -  4 vikombe
Siagi au mafuta - 1 kikombe
Maji - 2 vikombe
Chumvi - kiasi 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Weka vitu vyote katika bakuli. Kisha tia maji kiasi na uchanganye vizuri mpaka uwe unanata mkononi (Sticky). Mchanganyiko uwe mzito kidogo kuliko mchanganyiko wa kaimati.
  1. Uache utulie sehemu ya baridi muda wa nusu saa mpaka saa takriban. Ikiwa hali ya hewa ni joto, weka katika friji dakika chache tu.
  2. Weka chuma kikubwa cha tambarare (flat) kwenye moto wa kiasi, kisha teka mteko mkononi utandaze haraka katika chuma kiloshika moto, uzungushe unga mpaka ukamilishe duara la chuma. Au njia nyengine ni kuteka mteko mkononi kisha kuubandika unga na kubandua sehemu za chuma kote mpaka uenee katika chuma.
  1. Ukianza kugeuka rangi ya hudhurungi, kwangua unga unaozidi juu ya mkate utupe.
  1. Ubandue mkate uweke katika sahani ya kupakulia, nyunyizia samli ya kuyeyushwa kisha ikunje ukipenda kama kwenye picha.
  2. Endelea mpaka umalize mchanganyiko wa unga.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika) 
Vidokezo:   
  1. Mikate hii asili yake inatumiiwa unga wa barley (shayiri/talbiynah) ambao ni wa siha zaidi. Lakini unaweza kutumia unga mweupe au wa atta.
  2. Khubz raqaaiq umaarufu wake ni kuliwa kwa kuchanganywa na supu ya nyama au mchuzi chakula kinachoitwa ‘Thariyd’. Bonyeza upate upishi wa thariyd.
  1. Ikiwa chuma ni kipya, na mikate inaganda, changanya yai moja katika kipimo kisichokuwa na mafuta.
  2. Mikate ya Raqaaiq ina majina tofauti kama ifuatavyo:
Pande za Arabuni: Saudia, UAE, Kuwait = Khubz Raqaaiq
Waarabu wengine: Khubz Yaabis (Mkate mkavu) au Rakhaail
Wabulushi:  Timushi

0 Comments