November 13, 2017

MOLA WAKO ANAKUAMRISHA UWAFANYIE WEMA WAZAZI ILI AKULIPE PEPO

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلاَهُمَا فَلاَ تَقُل لَّهُمَآ أُفٍّ وَلاَ تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلاً كَرِيمًا))   ((وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا))  
((Na Mola wako Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima)) ((Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu,  Warehemu kama walivyonilea utotoni)) [Al-Israa:23-24]

Kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kumeungamana na kuwaheshimu wazazi kwani Allaah سبحانه وتعالىAmeamrisha kuwafanyia wema baada ya kuamrisha kumuabudu Yeye kama Alivyounganisha vile vile katika aya nyingine ya kumshukuru kwanza Yeye kisha wazazi:
((وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَى وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ))
((Na Tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni Kwangu Mimi ndiyo marudio)) [Luqmaan:14]
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametupa mafundisho katika Hadiyth zake nyingi kuhusu kuwaheshimu na kuwafanyia wema wazazi wetu:
 عن أنس وغيره: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم لما صعد المنبر قال: ((آمين آمين آمين)): فقالوا: يا رسول الله، علام أمنت؟ قال: ((أتاني جبريل فقال: يا محمد رغم أنف امرئ ذكرت عنده فلم يصل عليك، فقل: آمين. فقلت: آمين. ثم قال: رغم أنف امرئ دخل عليه شهر رمضان ثم خرج ولم يغفر له، قل: آمين. فقلت آمين. ثم قال: رغم أنف امرئ أدرك أبويه أو أحدهما فلم يدخلاه الجنة، قل: آمين. فقلت: آمين))
Kutoka kwa Anas na wengineo kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipanda katika minbar na akasema:((Aamiyn, Aamiyn, Aamiyn)). Akaulizwa: Ewe Mjumbe wa Allaah, mbona umesema Aamiyn? Akasema: ((Amenijia Jibriyl na kuniambia: "Ewe Muhammad, amekhasirika yule anayekusikia (unatajwa) na hakuswalii". Akasema: "Sema Aamiyn", ndio nikasema Aamiyn. Kisha akasema: "Amekhasirika unayemfikia mwezi wa Ramadhaan na ukaondoka naye hakughufuriwa" (dhambi zake). Akasema: "Sema Aamiyn", ndio nikasema Aamiyn. Kisha akasema: "Amekhasirika yule anayekuwa mkubwa kisha wazazi wake wawili au mmoja wao bado yu hai, na wasiwe sababu yake kuingia Peponi". Akasema: "Sema Aamiyn", ndio nikasema Aamiyn)) [Tuhfat Al-Ahwadhiy 5:550]
Hadiyth nyingine:
 عن أبي هريرة، رضي الله عنه، عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (( رغم أنف، ثم رغم أنف، ثم رغم أنف رجل أدرك والديه أحدهما أو كلاهما عند الكبر ولم يدخل الجنة))
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه  kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Amekhasirika, amekhasirika, amekhasirika, mtu ambaye wazazi wake wawili au mmoja wao wamefikia umri mkubwa (wa uzee) naye yu hai bado na haingii Peponi [kwa sababu ya kutowafanyia wema]))[Ahmad: 2:346] 
Kuwafanyia wema wazazi kunaendelea hata kama mzazi mmoja au wote wawili wamefariki, wema huo unaweza kuuendeleza kwa kuwaombea Du'aa, kuwatolea sadaka, kuwafanyia Hajj na kadhalika, na yote yamethibiti katika Sunnah.
Kwa hiyo kama tunavyoona umuhimu wa kuwaheshimu  wazazi wetu na kuwafanyia wema, basi tujitahidi kutekeleza amri za Mola wetu ili kupata Ridhaa Yake na Atulipe Pepo. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only