May 17, 2018

02-Fatwa: Kuacha Kufunga Ramadhwaan Kwa Ajili Ya Kazi Ngumu

Kuacha Kufunga Ramadhwaan Kwa Ajili Ya Kazi Ngumu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)


SWALI:

Yapi maoni yako kuhusu ugumu wa kazi ya mtu na ikawa vigumu kwake kufunga. Je inajuzu kwake kukata Swawm?

JIBU:

Maoni yangu ni yeye kuvunja Swawm yake kutokana kazi hii ni haraam kwake kuvunja Swawm, haijuzu kuacha kufunga. Haijuzu kwa mtu kulinganisha kazi yake na Swawm, anatakiwa kuchukua likizo kazini wakati wa Ramadhwaan, ili iwe kwake rahisi kuweza kufunga.
Swawm ya Ramadhwaan ni katika nguzo za Uislamu na haijuzu kwake kuacha kufunga (kwa sababu ya kazi).

[Hukumu ya Kiislamu juu ya nguzo za Uislamu, mj. 2, uk. 630]

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only