Kujitolea Kuwalisha Wenye Swawm Kwa Mali Ya Haraam
Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy
SWALI:
Kuna mtu anafanya kazi mahala panapouzwa pombe na anataka kuwafuturisha wafungaji masiku katika msikiti. Ipi hukumu ya hilo?
JIBU:
Ikijulikana mali yake ni katika njia hiyo ya haraam, kusiliwe chakula chake, kwa kuwa ni mali yajulikana wazi kuwa ni haraam. Jambo la pili ni kuwalisha wenye Swawm Misikitini ni kama kwamba mtu huyu anaona kuwa itamzidishia khayr na baraka ilihali sivyo ilivyo.
Post a Comment