May 19, 2018

Akiondoka Kabla Ya Imaam Kumaliza Rakaa 20 Na Akiswali Witr Nyumbani Atapata Fadhila Za Qiyaamul Layl?

SWALI:

As-salamu Aleikum,

Naomba munisimuliye kuhusu swalah ya taraweeh misikiti mengine wanaswali rakaa 23 na na mimi ni mtu wa kuswali 11 pamoja na witry kama ilivyo katika sunnah.Je nikiswali 8 pamoja na imam nikamaliziya witry nyumbani nitapata ujra huu alosema mtume sallahu alayhi wassallam.
kutokukamalisha Swalah ya taraawiyh na Imaam ili kupata fadhila za Qiyaamul-Layl kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema:


((Atakayesimama (kuswali) na Imaam hadi amalize ataandikiwa (fadhila za) Qiyaamul-Layl))[Imesimuliwa na at-Tirmidhiy na kaipa daraja ya Swahiyh al-Albaaniy katika Swahiyh at-Tirmidhiy]

 Sallahu Aleyhi Wasallam.
JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Tunashukuru kujua kwamba unafuatilizia vizuri na kwa karibu mafundisho
kwenye tovuti yako. Tunamuomba Allaah Akuzidishie elimu.

Kwa mujibu wa Hadiyth hiyo, tunaona kuwa hutokuwa umeswali na Imaam
hadi mwisho na hivyo kuweza kupata fadhila zilizotajwa humo kwani bado
Imaam atakuwa anaendelea kuswali sehemu ya Swalah hiyo na wewe ushaondoka.

Unachoweza kufanya ili usikose fadhila hizo, ni kama Maulamaa walivyoona kuwa unaweza baada ya Imaam kutoa Salaam katika Swalah ya Witr, wewe kunyanyuka na kuswali Rakaa moja ya kuitengua ile Witr na hapo utakuwa umefanya mawili kwa wakati mmoja. Utakuwa umekamilisha Swalah na Imaam hadi mwisho, na pia utaweza kwenda nyumbani kuswali Swalah yako ya Witr. Na hiyo ni kwa sababu hakuna Witr mbili katika usiku mmoja kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

((لا وتران في ليلة)) رواه الترمذي
((Hakuna Witri mbili katika usiku)) [At-Tirmidhiy]

Pia imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa baadhi ya nyakati si kila mara, akiswali Rakaa mbili baada ya kuswali Witr japokuwa alishasema kuwa Witr iwe ndio Swalah ya mwisho ya usiku.


Na Allaah Anajua zaidi  

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only