April 16, 2021

Hadiyth Zisizosihi Kuhusu Ramadhwaan


أحاديث لم تصح عن رمضانMkusanyaji: Abu Faatwimahwww.Uislamuwangu.blogspot.com

Tunamsifu Allaah, na tunamuomba msaada, na tunamuomba maghfirah, na tunatubu Kwake, na tunamuomba Atulinde na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu, Anayemuongoza Allaah hakuna wa kumpoteza, na Anayempoteza hakuna wa kumuongoza.Nashuhudia na nakiri kwamba hapana illaaha - muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali yakuwa peke Yake hana mshirika, na nashuhudia na nakiri kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mja Wake na ni Mjumbe Wake.Rahmah na Amani za Allaah zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyebalighisha yale yote aliyotakiwa kuyabalighisha kikamilifu; na Radhi za Allaah ziwe juu ya Swahaba zake waliofikisha kila walichopokea kutoka kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu kabisa katika ufikishaji hata ikafikia kwa mmoja wao kuhisi kuwa ni dhambi kubakia ndani ya moyo wake alichopokea kutoka kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya kukifikisha kwa ummah tena bila ya kuongeza wala kupunguza.Rahmah za Allaah ziwe juu ya Taabi’iyna na Taabi’ Taabi’iyna waliokuwa walinzi wa ‘Aqiydah na kila kilichopokelewa na kuhakikisha kuwa kinawafikia Waislamu kama alivyokibalighisha Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kama walivyopokea kutoka kwa Swahaba za Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya kumzulia uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na bila ya kubuni Hadiyth na kuzinasibisha kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).Maghfirah ya Allaah juu ya Muhaddithuwna waliozidhibiti na kuzihifadhi Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na kila uharibifu na uzushi.Nuru ya Allaah juu ya ‘Ulamaa walioweka misingi na kanuni za kuweza kuzitambua na kuziainisha Hadiyth sahihi za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na zile zisizo sahihi. Tawfiq ya Allaah kwa watakaowafuata kwa ihsaan mpaka siku ya Qiyamaah na kwa kila mwenye kutahadharisha ummah kutokana na Hadiyth zisizokuwa sahihi.إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله عليه وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار

Hakika maneno bora zaidi ni yale ya Allaah, na (hakika) uongofu bora zaidi ni ule wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); na shari ya mambo ni uzushi, na kila uzushi ni bid‘ah, na kila bid‘ah ni upotofu, na kila upotofu (mahali pake ni) Motoni.Ndugu zangu katika iymaan, napenda kujiusia nafsi yangu kwanza na kisha kuiusia nafsi yako kuwa na taqwa ya Allaah na kumtii Allaah na Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kutekeleza kila Aliloliamrisha kadiri ya uwezo wetu, na kujikataza na kila Alichokikataza mara moja.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

“Enyi mlioamini! Muogopeni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa na nyinyi ni Waislamu”[1]يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah Amekuwa juu yenu Mwenye kuchunga.” [2]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧١﴾

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya kweli (ya sawasawa). Atakutengenezeeni ‘amali zenu, na Atakughufurieni madhambi yenu; na yeyote yule anayemtii Allaah na Mjumbe Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafaniko makubwa.” [3]Ndugu yangu katika iymaan, tunaukaribia mwezi wa Ramadhwaan, mwezi wenye fadhila nyingi, mwezi ambao ndani yake tunasamehewa madhambi yetu, mwezi ambao hauna wenye kufanana naye katika miezi yote ya mwaka kwa mavuno na ujira, mwezi ambao hupatikana na kutekelezwa ndani yake nguzo moja katika nguzo za Uislamu, mwezi ambao ndani yake kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu, mwezi ambao ndani yake milango yote ya Jannah huwekwa wazi na milango ya Moto hufungwa, mwezi ambao mashaytwaan hufungwa minyororo, mwezi ambao katika kila usiku yake Allaah Huwatoa watu kwenye Moto wale waliostahiki kutupwa Motoni, mwezi wa Qur-aan, mwezi wa Rahmah, mwezi wa Maghfirah, mwezi wa Tawbah na mwezi wa Taraawiyh.Ndugu yangu katika iymaan, waraka huu wenye kuorodhesha na kubainisha baadhi ya Hadiyth zisizokuwa Sahihi umependekezwa kutokana na kuwa ndimi za watu wengi wa kawaida kwenye shughuli mbali mbali na mikusanyiko mingi husikikana zikitoa kauli nyingi na Hadiyth, kauli na Hadiyth ambazo huelezwa au husemwa kuwa ni kauli au Hadiyth Sahihi za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kama zile zenye kutaja na kueleza kuhusu fadhila za kusoma baadhi ya Suwrah za Qur-aan, au kusoma nyiradi fulani katika nyakati maalumu, au fadhila za Swawm ya baadhi ya miezi na masiku na kadhalika. Ndugu yangu katika iymaan, kwa watu wenye hali kama hiyo ya kupenda kueleza fadhila za kitu na kutoa ushahidi wa Hadiyth ni katika jambo jepesi kabisa na rahisi sana katika kuyatilia nguvu wanayoyasema ukilinganisha na kuyatolea ushahidi wa Qur-aan, yote kwa kuwa si tu inakubalika kuelezea Hadiyth kwa kuleta maana yake pekee bila ya kuitaja kwa tamshi lake lililothibiti, bali hakuna njia wala uwezekano wa watu wa kawaida walio wengi tena bila ya ujuzi wowote ule kudhibiti Hadiyth kwa wingi wake. Pia huwa wanatoa ushahidi wa Hadiyth kwa kuelewa kuwa haikubaliki kutoa ushahidi wa Aayah ya Qur-aan kwa maana yake kama ni dalili ya ushahidi wa chochote kile isipokuwa iwe kwa lafdhi yake kama ilivyoteremshwa kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).Ndugu yangu katika iymaan, mara nyingi na ndio ukweli kuwa watu wengi wa kawaida husikiliza sana Madu’aat na Wu’aadh -wenye kutoa mawaidha- ukilinganisha na usikilizaji wao wa Maulamaa na Wanavyuoni; hivyo kwa kusikiliza sana Madu’aat na Wu’aadh wameweza kwa namna fulani kurithi kutoka kwao jumla isiyokuwa ndogo ya Hadiyth Dhwa’iyf[4], na Mawdhwuw’’[5], na Matruwkah[6] –zilizoachwa-, na Munkarah[7] na wala sio nyepesi; yote kwa kuwa katika ‘Ulamaa kuna kundi lenye kufuata dhehebu linalokubalisha na kujuzisha utumiaji wa Hadiyth Dhwa’iyf katika fadhila za ‘amali, hivyo huwa hawaoni haraj wala tabu wala karaha wala ubaya wala dhambi katika utumiaji wa Hadiyth hizi na kuwasikilizisha watu wa kawaida hasa zikiwa ziko mbali na hukumu za kivitendo na misingi ya ‘Aqiydah pamoja na kuwa wale wenye kufuata dhehebu hilo katika Maulamaa wameshurutisha kuwa katika kukubalika utumiaji wa Hadiyth Dhwa’iyf ni lazima mtumiaji abainishe wakati anapozitumia na kuzieleza udhaifu wake ili msikilizaji asije kuona wala kudhania wala kuamini kuwa ni Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumpelekea kuzinasibisha nae.Ndugu yangu katika iymaan, kinachojitokea na ndio kilichopo ni kuwa hakuna mwenye kushikamana na utekelezaji wa hilo sharti la kubainisha udhaifu wa Hadiyth Dhwa’iyf wakati zinapotumiwa isipokuwa wale Aliowarehemu Allaah, bali wakati wote na hili ndio hasa linaloeleweka ni kuwa mtumiaji wa Hadiyth zisizokuwa sahihi huwa ni mwenye kuzitetea hizo Hadiyth kwa kueleza kuwa hakuna ubaya ndani yake na ndio zikaitwa Hadiyth na kuwa zimetumiwa na bado zinaendela kutumiwa na wahadhiri wengi.Ndugu yangu katika iymaan, ni bora tuwe pamoja na lile kundi lisilojuzisha wala kukubalisha utumiaji wa aina yoyote na wowote ule wa Hadiyth Dhwa’iyf ni sawa sawa iwe katika yenye kuhusiana na yale ya kidunia au yale ya ki-Dini, si katika ‘Aqiydah wala si katika hukumu, si katika fadhila za ‘amali wala si katika chochote kile; yote kwa kuwa ziko Hadiyth Swahiyh za kutosheleza katika kila kinachohitajika ambazo zinapelekea kutokuwa na haja ya kutumia Hadiyth Dhwa’iyf wachila mbali kutumia Ahaadiyth Mawdhwuw’ah.Ndugu yangu katika iymaan, wakati wote huo wasikilizaji au walengwa huwa ni katika lile kundi lisilokuwa na uwezo wowote ule wa kufikia kuelewa kuwa muhadhiri wao anawapandikizia mambo ambayo hayakuthibiti bali ni ya uongo na ni ya kutungwa na kwamba mhadhiri wao wakati huo huo huwa anamzulia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), mtu ambaye hatakiwi wala hatazamiwi kuzuliwa kwani huko ni kuangamia na kujiandalia makaazi Motoni.Ndugu yangu katika iymaan, Hadiyth hizi zisizokuwa sahihi ambazo hutoka kwenye midomo ya baadhi ya wahadhiri kama hazikuanikwa na kubainishwa kwenye jamii yetu huenda Waislamu walio wengi kwenye hii jamii yetu wakaja kudhania na kupelekea kuamini kuwa ni miongoni mwa Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwamba yanayoelezwa ndani ya Hadiyth hizo -za kutungwa na za uongo- ni sehemu ya Dini, na ukweli ni kuwa haya ndiyo hasa yanayopatikanwa na kudhihirika kwenye jamii yetu na nyingine nyingi tu za Waislamu wasiokuwa tayari kuchagua ni mhadhiri gani wa kumsikiliza na ni muhaadharah gani wa kuusikiliza kwa kusahau agizo na ushauri muhimu wa Salaf wa ummah wenye kuwataka wawe na tahadhari katika uchukuaji wa -elimu ya- Dini yao, kama alivyoshauri Imaam Muhammad bin Siyriyn (Rahimahu Allaah) kwa kusema:“Hili ni jambo au hii ni elimu ya Dini, hivyo kuwa muangalifu sana ni kutoka kwa nani unaichukua Dini yako."Ndugu yangu katika iymaan, ni kutokana na hilo ndio ikapendekezwa kazi hii ya kuzikusanya baadhi ya Hadiyth zisizokuwa sahihi hasa kwenye Swawm kwanza na ni matarajio yangu kuwa kutapatikana wasaa mwingine in shaa Allaah wa kuzikusanya Hadiyth nyinginezo zisizokuwa sahihi kwenye milango mingine isiyokuwa Swawm.Ndugu yangu katika iymaan, si jambo linalokubalika hata kidogo kwenye Uislamu kwa mtu yeyote yule wachilia mbali wahadhiri kutumia Hadiyth zenye kueleweka kuwa ni miongoni mwa Hadiyth zisizokuwa sahihi kwani ni za kutunga zenye kumzulia uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwapelekea Waislamu kuona kuwa ni Hadiyth zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwapelekea kudhania kuwa ni Hadiyth Swahiyh na kushikamana na yale yanayoelezwa na Hadiyth husika.Ndugu yangu katika iymaan, Hadiyth hizi za kutungwa na za uongo ambazo kwa ukweli zimezagaa kwenye jamii yetu na jamii nyinginezo za Kiislamu ni hatari mno kwa ummah, hasa hasa zile zenye kuanzisha na kuchochea mambo ya bid’ah (uzushi), kufuru, ushirikina, ubaguzi, uzalendo na kadhalika.Ndugu yangu katika iymaan, kubwa zaidi ya hayo na ndio la kuzingatiwa na kila mmoja wetu na hasa wale wenye kutumia Hadiyth hizi za kutungwa na za uongo ni kuwa, imethibiti kemeo kali bali imethibiti wapi yatakuwa makaazi yake kwa kumzulia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye Hadiyth zilizo sahihi kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:“Yeyote yule atayenizulia uongo, basi ajiandalie makaazi yake Motoni.” [8]

Pia imethibiti kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Mwenye kunizulia  uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makaazi yake Motoni.” [9]Pia imethibiti kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Msinizulie, kwani yeyote yule atayenizulia uongo, basi atauingia Moto.” [10]Pia imethibiti kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Hakika kunizulia uongo mimi, sio sawa kama kumzulia uongo mmoja yeyoye yule, -hivyo basi-yeyote yule atayenizulia uongo, basi ajiandalie makaazi yake Motoni.”[11]

Ndugu yangu katika iymaan, kutokana na hali hiyo iliyothibiti kwenye Hadiyth Swahiyh Muhaddithuwna wametofautiana kuhusu hukumu ya mwenye kumzulia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); hata hivyo ni vyema ieleweke kuwa kumzulia Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni sawa na kumzulia Allaah kwa kuwa yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuletwa isipokuwa kubalighisha Ujumbe wa Allaah. Hivyo, mtu anapomzulia Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huwa kiuhakika anamzulia Yule Aliyemtuma kubalighisha Ujume Wake na sio mjumbe mwenyewe.Ndugu yangu katika iymaan, kutokana na hali hiyo iliyothibiti kwenye Hadiyth Swahiyh Muhaddithuwna kwa tawfiq Yake Mola wa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wamechukuwa juhudi za hali ya pekee zenye lengo la kuuokoa ummah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na makaazi ya Motoni kwa kuzifuatilia kwa uchambuzi na uchunguzi wa kina Hadiyth karibu zote za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuziwekea elimu maalumu –‘Uluwmul Hadiyth-; pia Muhaddithuwna kwa tawfiq Yake Mola wa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wamesimama kidete kwa juhudi kubwa zaidi kuweka misingi ya taaluma –Mustwalahul-Hadiyth[12]- yenye kanuni ambayo inapambanua Hadiyth Swahiyh za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ambazo sio sahihi.Ndugu yangu katika iymaan, kwa ufupi kanuni hizo zinapelekea kwanza kuangalia uthibiti wa kila Hadiyth kutokana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kuwa si kila Hadiyth inayonasibishwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) -kama mada yetu inavyojaribu kueleza- ni Swahihi, na kama inavyojitokeza na ndio kusudio la waraka huu kuna Hadiyth nyingi zinazonasibishwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ilhali hazijathibiti wala hazitokani kamwe na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bali ni za kutungwa na ni za kumzulia uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).Ndugu yangu katika iymaan, pia Muhaddithuwna kwa tawfiq Yake Mola wa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wameweza kufikia kuangalia uadilifu wa Hadiyth husika katika hukumu husika (yaani je, Hadiyth hiyo inanasibiana na hukumu hiyo au la?) na kutambua Hadiyth zilizothibiti na daraja zake na wakati huo huo kuweza kuzitenga na kuziweka mbali zile zisizothibiti kwa kuainisha tatizo lake na kutahadharisha ummah ubaya wake kwa kuzipa jina lenye kuashiria kuwa ni Hadiyth za kutunga.Ndugu yangu katika iymaan, Hadiyth hizi na nyingine kama hizo, ambazo sikuwafikishwa kuzitaja katika waraka huu ni zenye kueleweka kwa wahusika wake, kuwa sio Hadiyth na kama Hadiyth basi ni Dhwa’iyf, au Mawdhwuw’, au Matruwk –zilizoachwa-, au Munkar; hivyo ni vyema kutozitumia kwani si Hadiyth Swahiyh, na kuzitumia kama ni Hadiyth baada ya kuthibiti kuwa sio, ni kumzulia uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyothibiti katika Hadiyth sahihi kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Yeyote yule atayehadithia kuhusu mimi Hadiyth hali ya kuwa anaona kuwa ni –ya- uongo, basi yeye ni mmoja miongoni mwa hao waongo.”[13]Ndugu yangu katika iymaan, vipi tutakuwa miongoni mwa mwenye kutarajia kutekeleza na kukubaliwa ‘ibaadah zetu ikiwemo hii ya Swawm huku tukiwa miongoni mwa wale wenye kumzulia au wenye kuwasikiliza wahadhiri wenye kumnasibisha aliyekuwa akihuzunishwa sana na yanayotutaabisha; aliyekuwa akituhangaikia sana mimi na wewe -na Waumini wote kwa ujumla- kama hatutokuwa miongoni mwa wenye kumzulia uongo au wenye kusikiliza wenye kumnasibisha na yasiyothibiti kuwa ameyasema ni mpole na mwenye huruma sana.Ndugu yangu katika iymaan, ningependa kwa at-Tawfiyq yake Mola wa Ramadhwaan kujaalia miongoni mwa ya kukaribishia Ramadhwaan huku kubainisha na kuainisha kwa kutaja baadhi ya Hadiyth zisizokuwa sahihi zilizo mashuhuri katika ndimi za wahadhiri wetu wengi, huku nikijaribu kadiri ya nitakavyowafikishwa kuthibitisha kauli za wenye elimu kuhusiana na hukumu za Hadiyth. Ni wajibu wa kila mwenye elimu kuifikisha elimu hiyo kwa Waislamu na ni wajibu wa kila mwenye kuelewa kutokujuzu kwa jambo fulani kulibalighisha hilo jambo na kuhakikisha kuwa ummah unatahadharishwa nalo na huko ndiko katika iymaan na huko ndiko katika kuokoana na Moto.

Miongoni mwa hizo Hadiyth ni:

اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان

وقد ضعّفه الألباني في "ضعيف الجامع الصغير“Ewe Mola Tubarikie katika –mwezi wa- Rajab na –mwezi wa- Sha’abaan na Tubalighishe –mwezi wa- Ramadhwaan.”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.شعبان شهري، ورمضان شهر الله، وشعبان المطهر، ورمضان المكفر

ضعّفه الألباني في السلسلة الضعيفة.“Sha’abaan ni mwezi wangu, na Ramadhwaan ni mwezi wa Allaah, na Sha’abaan inatwahirisha, na Ramadhwaan inafuta (madhambi)”

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni dhaifu kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah." رجب شهر الله، وشعبان شهري، ورمضان شهر أمتي"

ضعيف ، نص الشيخ الألباني على تضعيفه في السلسلة الضعيفة

“Rajab ni mwezi wa Allaah, na Sha’abaan ni mwezi wangu, na Ramadhwaan ni mwezi wa ummah wangu”

Hadiyth Dhwa’iyf, ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.لو يعلم العباد ما في رمضان لتمنت أمتي أن تكون السنة كلها رمضان...

 موضوع ( يعني مكذوب على النبي صلى الله عليه وسلم) قال بذلك ابن الجوزي والألباني وغيرهما. وقال ابن حجر عنه : ضعيف جدا.“Lau wangeelewa waja yaliyomo katika Ramadhwaan, ummah wangu ungalitamani iwe Ramadhwaan mwaka mzima...”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (yaani amezuliwa uongo Mtume wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivyo Ibn Aj-Jawzy na Al-Albaaniy na wengineo, na amesema Ibn Hajar kuwa ni Hadiyth dhaifu sana.لا تقولوا رمضان، فإن رمضان اسم من أسماء الله تعالى، ولكن قولوا: شهر رمضان

  والحديث موضوع”  ترتيب الموضوعات " للذهبي، " الفوائد المجموعة“  للشوكاني“Msiuite –mwezi kwa jina la- Ramadhwaan; kwani Ramadhwaan ni jina katika Majina ya Allaah, lakini semeni mwezi wa Ramadhwaan.”

Hadiyth hii ni Hadiyth Mawdhwuw’ –ya kutungwa- amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imetajwa kwenye kitabu cha Imaam Adh-Dhahabiy cha Hadiyth za kutungwa na kwenye kitabu cha Ash-Shawkaaniy pia kiitwacho Al-Fawaaid.

"يا أيها الناس قد أظلكم شهر عظيم ، شهر فيه ليلة خير من ألف شهر ، جعل الله صيامه فريضة ، وقيام ليله تطوعا ، من تقرب فيه بخصلة من الخير كان كمن أدى فريضة فيما سواه ، ومن أدى فيه فريضة كان كمن أدى سبعين فريضة فيما سواه ، وهو شهر الصبر ، والصبر ثوابه الجنة ، وشهر المواساة ، وشهر يزاد فيه في رزق المؤمن ، ومن فطر فيه صائما كان مغفرة لذنوبه وعتق رقبته من النار ، وكان له مثل أجره من غير أن ينتقص من أجره شيء . قالوا : يا رسول الله ، ليس كلنا يجد ما يفطر الصائم ، قال : يعطي الله هذا الثواب من فطر صائما على مذقة لبن ، أو تمرة ، أو شربة من ماء ، ومن أشبع صائما سقاه الله من الحوض شربة لا يظمأ حتى يدخل الجنة ، وهو شهر أوله رحمة ، ووسطه مغفرة ، وآخره عتق من النار ، فاستكثروا فيه من أربع خصال ، خصلتان ترضون بهما ربكم ، وخصلتان لا غنى بكم عنهما ، أما الخصلتان اللتان ترضون بهما ربكم فشهادة أن لا إله إلا الله ، وتستغفرونه ، وأما الخصلتان اللتان لا غنى بكم عنهما ، فتسألون الجنة ، وتعوذون من النار".

وهو حديث ضعيف لا تقوم به حجة. رواه البيهقي ، وضعفه الألباني في "المشكاة"، وقال: منكر في " السلسلة الضعيفة"

Alitukhutubia Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku ya mwisho ya mwezi wa Sha’abaan; akasema: "Enyi watu! Umekufikieni mwezi ‘adhimu –na kuna riwaayah nyingine ambayo pia ni ya kutungwa kumeengezwa ‘wenye baraka’-, mwezi ndani yake kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu; Allaah Amejaalia Swawm yake -mwezi huu- kuwa ni fardhi (wajibu)-, na kisimamo (qiyaam) chake- cha usiku wake ni tatwawwu’u –kujitolea: sio fardhi wala sio wajibu-, atakayejikurubisha ndani yake –ndani ya mwezi huu- kwa jambo lolote lile la kheri, basi -jazaa yake- huwa kama mtu aliyetekeleza fardhi katika mwezi mingine usiokuwa huu, na atakayetekeleza fardhi ndani yake –ndani ya mwezi huu-, basi -jazaa yake- huwa kama mtu aliyetekeleza fardhi sabini (70) katika mwezi mingine usiokuwa huu, nao ni mwezi wa Swabr (subira), na subira thawabu yake ni Jannah, na ni mwezi ambao ndani yake riziki ya Muumini huzidishwa, na yeyote yule atakayemfuturisha mfungaji ndani yake, basi -jazaa yake itakuwa ni- maghfirah ya madhambi yake, na kuachwa huru shingo yake na Moto, na atapata ujira kama aupatao mfungaji bila ya kupungua chochote katika ujira wake –mfungaji.” Tukasema: Ee Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), sio sote tunaweza kupata cha kumfuturisha huyo mfungaji; Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawajibu: "Allaah Humpa thawabu hizi yule atakayemfuturisha mfungaji kwa funda la maziwa au kwa -kokwa ya- tende au kwa funda la maji; na atakayemshibisha mfungaji basi Allaah Atamnywesha katika hodhi funda ambalo hatopata kiu baada yake mpaka aingie Jannah; nao ni mwezi -ambao- mwanzo wake ni rahmah, na katikati yake ni maghfirah, na mwisho wake ni kuachwa huru kutokana na Moto. -na kuna riwaayah nyingine ambayo pia ni ya kutungwa kumeengezwa- na atakayempunguzia kazi mtumishi -mfanyakazi wake- ndani ya mwezi huu, Allaah Atamghufuria madhambi yake na kumuacha huru na Moto-; basi kithirisheni sana ndani yake mambo manne, mtamridhisha Mola wenu kwayo na mawili mengine hamjikwasi -hamna budi- nayo; ama yale mawili ambayo mtakayoridhisha nayo Mola wenu ni shahada (kushuhudia kwamba hapana Mola muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) na mumtake maghfirah, na ama yale mawili mengine ambayo hamna budi nayo ni kuomba Jannah na kujilinda -kujikinga kwake na –adhabu- ya Moto".

Hadiyth hii ni Dhwa’iyf haiwezi kuwa hoja wala dalili. Ameipokea Al-Bayhaqiyy na akaidhoofisha kwa kusema Dhwa’iyf Shaykh Al-Albaaniy kwenye Al-Mishkaat na akasema ni Hadiyth Munkar kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.Ndugu yangu katika iymaan, hii Hadiyth si katika Hadiyth zenye kueleza kuhusu fadhila za ‘amali hata ifanyiwe kazi au itumike kwa msimamo wa wale wenye kukubali utumiaji wa Hadiyth Dhwa’iyf kwa sharti lao waliloliweka, ukweli ni kuwa Hadiyth hii inathibitisha na kuweka hukumu nyingi tu –kama tulivyoziona- miongoni mwake: Jazaa -au thawabu- ya utekelezaji wa fardhi ndani ya mwezi wa Ramadhwaan ni sawa na jazaa ya utekelezaji fardhi sabini (70) katika mwezi mwengine usiokuwa Ramadhwaan, na kwamba thawabu za Naafilah -Sunnah- ndani yake ni sawa na thawabu za fardhi katika mwezi mwengine usiokuwa Ramadhwaan, na kwamba thawabu za kumfuturisha mfungaji ni kusamehewa yule aliyefutarisha madhambi yake, na kwamba thawabu hizi huwa kwa kila aliyefuturisha mfungaji kwa funda la maziwa au kwa -kokwa ya- tende au kwa funda la maji; ndio utaona watu wengi wanashindana na kukimbilia kwenye kuwa wa kwanza katika wenye kuwafikishia wafungaji tende au kokwa za tende na wala hawajali wala hawashughuliki na yale yenye kuweza kumshibisha mfungaji aliye fakiri, inawatosheleza kuwa walimlisha kokwa moja ya tende au mbili au tatu wakati wa kufungua kinywa; na hukumu nyinginezo kama tulivyoziona, hukumu ambazo hakuna njia ya kuthibiti na kukubalika isipokuwa kwa njia ya Hadiyth Swahiyhadiythi Swahiyhah au kwa uchache basi Hadiyth Hasan.أول شهر رمضان رحمة ، وأوسطه مغفرة ، وأخره عتق من النا

ضعيف أشار ابن خزيمة إلى تضعيفه، وقال الشيخ الألباني: إنه حديث منكر.“Mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan ni rahmah, na katikati yake ni maghfirah, na mwisho wake ni kutolewa kwenye Moto”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf; Ibn Khuzaymah ameashiria kuwa ni Hadiyth Dhwa’iyf, na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hadiyth Munkar.خمس يفطِّرن الصائم وينقضن الوضوء : الكذب ، والنميمة ، والغيبة ، والنظر بشهوة ، واليمين الكاذبة

موضوع. قال ابن أبي حاتم : سألت أبي عن هذا الحديث فقال: هذا حديثُ كَذِبٍ، وقال بوضعه الشيخ الألباني في ضعيف الجامع وليس معنى هذا التساهل في هذه المحرمات ، فإنها تفطر الصائم وتوجب القضاء عند ابن حزم والإمام الأوزاعي (خلافا لجمهور أهل العلم)، وتنقص الأجر بل ربما نسفته عند بقية الأئمة، ولكن المقصود أن نسبة هذا اللفظ إلى النبي صلى الله عليه وسلم لا تجوز.

“Mambo matano yanamfunguza mfungaji na yanabatilisha wudhuu: Kusema uongo, kufitinisha, kusengenya, kutazama kwa matamanio, kula yamini ya uongo.”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ amesema Ibn Abi Haatim: Nilimuuliza baba yangu kuhusiana na Hadiyth hii, akasema: Hii ni Hadiyth ya uongo; na aliyesema kuwa imetungwa ni Shaykh Al-Albaaniy katika Dhwa’iyful Jaami’.  Kusema kwao huko hakuna maana kuwa haya mambo ya haramu yaliyotajwa yamedharauliwa, ukweli ni kuwa yanabatilisha Swawm na kuwajibika kulipwa kwa hiyo Swawm kwa kauli ya Ibn Haazim na Imaamu al Awzaa’iy  -kinyume na jamhuri ya Wanachuoni-, na bila ya shaka yoyote ile yanapelekea kupunguka kwa thawabu za Swawm, lakini kilichokusudiwa na ndio waraka huu unakieleza ni kuwa kulinasibisha lafdhi hili kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuzuju wala hakukubaliki kwani hakulitamka.أن امرأتين صامتا وأن رجلاً قال: يا رسول الله إن هاهنا امرأتين قد صامتا وإنهما قد كادتا أن تموتا من العطش فأعرض عنه أو سكت ثم عاد وأراه قال بالهاجرة قال يا نبي الله إنهما والله قد ماتتا أو كادتا أن تموتا قال ادعهما قال فجاءتا قال فجيء بقدح أو عس فقال لإحداهما: قيئي فقاءت قيحاً أو دماً وصديداً ولحماً حتى قاءت نصف القدح ثم قال للأخرى: قيئي فقاءت من قيحٍ ودمٍ وصديدٍ ولحمٍ عبيطٍ وغيره
حتى ملأت القدح ثم قال إن هاتين صامتا عما أحل الله وأفطرتا على ما حرم الله عز وجل عليهما جلست إحداهما إلى الأخرى فجعلتا يأكلان لحوم الناس.

الضعيفة"

“Wanawake wawili walifunga – katika uhai wa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- na kwamba mtu alisema: Ee Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)! Hakika wanawake wawili hawa wamefunga na kwamba wao wawili walikaribia kufa kwa kiu; -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- akampuuza au alinyamaza kimya; kisha –yule mtu- akarejea… akasema: Ee Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)! Hakika wawili hao wamekwisha kufa au wanakaribia kufa –akitafuta wapewe rukhsa ya kufungua kwa hali yao mbaya-; -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- akasema: Waiteni. Akasema: Wakaja wote wawili; akasema: kikaletwa chombo na akaambiwa mmoja wao: Tapika ndani yake yale mliyokuwa mkila. Basi alitapika matapishi au damu na usaha na nyama, alitapika mpaka kile chombo kikajaa nusu yake, na kisha akamwambia yule mwengine -wa pili wao-: Tapika, basi na yeye alitapika matapishi na damu na usaha na nyama  na mengineo mpaka chombo kikajaa, kisha -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- akasema: Hakika wanawake wawili hawa walifunga –kwa kujizuilia kutokula- kutokana na yale Aliyoyahalalisha Allaah, na wakafungua Swawm zao  kutokana na yale Aliyowaharamishia Allaah, alikaa mmoja wa wawili hawa kwa mwenzake wakawa wanakula nyama za watu (wanasengenya).”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf.نوم الصائم عبادة ، وصمته تسبيح، وعمله مضاعف، ودعاؤه مستجاب، وذنبه مغفور

وهو حديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".“Usingizi wa mwenye kufunga ni ‘ibaadah, na kunyamaza kwake kimya (kutokusema kwake) ni tasbiyh, na ‘amali yake ni yenye kuongezwa maradufu, na du’aa yake ni yenye kutakabaliwa, na dhambi zake ni zenye kughufuriwa.”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.نوم الصائم عبادة"

ضعيف، نص على تضعيفه الألباني في السلسلة الضعيفة

“Usingizi wa mwenye kufunga ni ‘ibaadah”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf, amesema hivyo Shaykh Al-Albaaniy kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

صوموا تصحوا

وهو حديث ضعيف ، وإن كان معناه صحيحاً ، وقد ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

“Fungeni mtapata siha (afya).”

Ni Hadiyth dhaifu japokuwa maana yake sahihi; ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.

يوم صومكم يوم نحركم

قال عنه السيوطي في الآلئ : كذب ، لا أصل له. وسبقه إلى ذلك الإمام أحمد بن حنبل كما نقل السخاوي في المقاصد.“Siku ya Swawm yenu (kufunga kwenu) siku ya kuchinja kwenu.”

Amesema Imaam As-Suyuutwiy: Hadiyth hii haina asli, na alimtangulia kwa hayo Imaam Ahmad bin Hanbal kama alivyonukuu As-Sakhaawiy kwenye Al-Maqaaswid.لا تزال أمتي بخير ما أخَّروا السحور وعجَّلوا الفطر

رواه أحمد والحديث منكر كما قال الشيخ الألباني، والصحيح من ذلك حديث:

لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الْفِطْرَ

“Ummah wangu utaendelea kuwa katika kheri madhali wanachelewesha Suhuwr (kula daku) na wanaharakisha kufungua kinywa.”

Ameipokea Ahmad na Hadiyth ni Munkar kama alivyosema Shaykh Al-Albaaniy; na kilicho sahihi katika Hadiyth hiyo ni:“Watu wataendelea kuwa katika kheri madhali watakuwa wanaharakisha kufutari.” [14]

أعطيت أمتي في شهر رمضان خمسا لم يعطهن نبي قبلي أما واحدة ؛ فإنه إذا كان أول ليلة من شهر رمضان ينظر الله
عز وجل إليهم، ومن نظر الله إليه لم يعذبه

وأما الثانية ؛ فإن خلوف أفواههم حين يمسون أطيب عند الله من ريح المسك

وأما الثالثة ؛ فإن الملائكة تستغفر لهم في كل يوم وليلة

وأما الرابعة فإن الله عز وجل يأمر جنته فيقول لها: استعدي وتزيني لعبادي، أوشك أن يستريحوا من تعب الدنيا إلى داري وكرامتي

وأما الخامسة ؛ فإنه إذا كان آخر ليلة غفر الله لهم جميعا
فقال رجل من القوم: أهي ليلة القدر؟ فقال: لا، ألم تر إلى العمال يعملون،
فإذا فرغوا من أعمالهم وفوا أجورهم " وفي لفظ (تستغفر لهم الحيتان
ذكره العلامة الألباني في سلسلته الضعيفة وقال في المشكاة فيه هشام ابن أبي هشام ضعيف إتفاقا وهو متروك“Ummah wangu umepewa mambo matano kwenye Ramadhwaan hajapewa Mtume yeyoye yule kabla yangu; Jambo la kwanza, Unapokuwa usiku wa kwanza kwenye mwezi wa Ramadhwaan Allaah Huwatazama –ummah wangu- na anayetazamwa na Allaah Hatomuadhibu.

Jambo la pili, harufu ya vinywa vyao inapendeza zaidi kwa Allaah kuliko harufu ya miski.

Jambo la tatu, Malaika wanawaombea maghfirah kila siku mchana na usiku.

Jambo la nne, Allaah Huamrisha Jannah Yake kwa kuiambia: Jiandae na jipambe kwa ajili ya waja Wangu, karibu watapumzika kutokana na taabu za dunia na kwenda kwenye Nyumba Yangu na kwenye Karama (utukufu) Yangu.

Jambo la tano, na inapokuwa mwisho wa usiku Allaah Huwaghufuria wote. Akauliza mtu: je, huu ndio usiku wa Laylatul Qadr? -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- akasema: Sio; je, huoni kuwa wafanyakazi hufanya kazi na wanapomaliza kazi yao hulipwa ujira wao. Na katika riwaayah: Samaki huwaombea maghfirah.”

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Dhwa’iyf kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na pia akasema kwenye Al-Mishkaat kuwa ndani yake yuko Hishaam bin Abi Hishaam ambaye ni Dhwa’iyf kwa maafikiano na ni Matruwk (aliyeachwa Hadiyth zake).إذا كان أول ليلة من شهر رمضان نظر الله عز وجل إلى خلقه، وإذا نظر الله عز وجل إلى عبده لم يعذبه أبدا، ولله عز وجل فى كل ليلة ألف ألف عتيق من النار

موضوع (يعني مكذوب على النبي صلى الله عليه وسلم) قال بذلك ابن الجوزي، والألباني في السلسلة الضعيفة

“Inapokuwa usiku wa mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan Allaah Huwatazama viumbe Wake, na Allaah Anapomtazama mja Wake Hatomuadhibu abadan; na Allaah Huwatoa Motoni katika kila usiku elfu elfu.”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ –ya kutungwa- amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivyo Ibn Al-Jawziy na Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.يستقبلكم وتستقبلون ثلاث مرات، فقال عمر بن الخطاب: يا رسول الله وحيٌ نزل؟ قال: لا. قال: عدوٌ حضر؟ قال: لا. قال: فماذا؟ قال عليه الصلاة والسلام: إن الله عز وجل يغفر في أول ليلة من شهر رمضان لكل أهل هذه القبلة.

وقال عنه الألباني: منكر، وذلك في "ضعيف الترغيب والترهيب".“Atakupokeeni na -nyinyi- mtampokea” mara tatu, ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)! Ni Wahyi umeteremshwa? -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)- akasema: Sio. ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Je, ni adui amehudhuria?  -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)- akasema: Sio. ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Basi nini? -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)- akasema: Hakika Allaah Anawaghufuria katika usiku wa mwanzo wa Ramadhwaan kwa kila mmoja wa katika kabila hili.”Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Munkar kwenye Dhwa’iyf At-Targhiyb wat-Tarhiyb.إن للصائم عند فطره دعوة لا ترد

ضعيف ، أشار إلى ضعفه ابن القيم في زاد المعاد، ونص على تضعيفه الشيخ الألباني في تمام المنة وغيره، وفي الصحيح غنية، فقد صح أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال :( ثلاثة لا ترد دعوتهم: الصائم حتى يفطر والإمام العادل ودعوة المظلوم) صححه الألباني في السلسلة الصحيحة ، وشتان بين اللفظين.

“Hakika kwa mwenye kufunga wakati wa kufutari du’aa hairejeshwi (haikataliwi).”Ni Hadiyth Dhwa’iyf, ameashiria hayo Ibn Al-Qayyim kwenye Zaad Al-Ma’aad na pia Shaykh Al-Albaaniy kwenye Tamaam Al-Minnah na na kwengineko, na katika Sahihi kuna zenye kutosheleza, imethibiti kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:“Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“(Watu) watatu du'aa zao hazirudi: Mwenye kufunga hadi afuturu (afutari), Kiongozi muadilifu na du’aa ya aliyedhulumiwa…” [15]Amesema Al-Albaaniy ni Hadiyth Sahihi  kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah, umbali ulioje baina ya lafdhi mbili hizi.كان إذا دخل رمضان شد مئزره ، ثم لم يأتِ فراشه حتى ينسلخ

الحديث ضعَّفه الألباني بهذا اللفظ، قال: والشطر الأول منه صحيح بلفظ: (كان إذا دخل العشر شد مئزره، وأحيا ليلة، وأيقظ أهله) وهو في الصحيحين.“Alikuwa -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)- inapoingia Ramadhwaan akikaza shuka yake, kisha hakiendei kitanda chake (halali tena) mpaka –Ramadhwaan- imalizike”

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Dhwa’iyf kwa lafdhi hili, na akasema kuwa: Sehemu –nusu- ya pili ya Hadiyth ndio sahihi kwa lafdhi:"Alikuwa -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)- linapoingia kumi -la mwisho la Ramadhwaan; alikuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- akikaza shuka yake -makusudio hapa ni kuwa alikuwa akijibidiisha sana au akijiepusha na wake zake-, na akihuisha usiku -kwa kufanya ‘ibaadah-, na akiamsha ahli zake.” [16]صائم رمضان في السفر كالمفطر في الحضر

وهو حديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

“Mwenye kufunga Ramadhwaan kwenye safari ni sawa asiyefunga -hali-akiwa mkaazi.”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyful Jaami’ Asw Swaghiyr.انبسطوا في النفقة في شهر رمضان، فإن النفقة فيه كالنفقة في سبيل الله

وهو حديث ضعيف، كما قال الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير" نص على نكارته الألباني في السلسلة الضعيفة.

“Kunjuweni kwenye utoaji katika mwezi wa Ramadhwaan, kwani utoaji ndani yake ni kama utoaji kwenye Njia ya Allaah.”

Ni Hadiyth dhaifu kama alivyosema Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr na kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah amesema kuwa ni Munkar.من أدرك رمضان وعليه من رمضان شيء لم يقضه، فإنه لا يقبل منه حتى يصومه

ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

“Mwenye kukutana na Ramadhwaan huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulilipa, basi haitokubaliwa Swawm yake mpaka alipe ile anayodaiwa.”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.من أدرك رمضان وعليه من رمضان شيء لم يقضه ، لم يتقبل منه، ومن صام تطوعاً وعليه من رمضان شيء لم يقضه، فإنه لا يتقبل منه حتى يصومه

 والحديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "سلسلة الأحاديث الضعيفة".

“Mwenye kukutana na Ramadhwaan huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulilipa, basi haitokubaliwa kwake, na atayefunga Swawm ya kujitolea (isio za faradhi wala wajibu) huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulikidhi (hakulilipa) basi haitokubaliwa kwake mpaka –kwanza- aifunge -ile siku anayodaiwa ya –Ramadhwaan.”

Hadiyth ni Dhwa’iyf. Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni dhaifu kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

من أفطر يوما من رمضان في غير رخصة رخصها الله له لم يقض عنه صيام الدهر كله وإن صامه

ضعيف، وقد أشار لذلك البخاري وضعفه الألباني في مشكاة المصابيح  

“Mwenye kula siku -moja- katika Ramadhwaan bila ya rukhsa (udhuru) yoyote ile Aliyoiruhusu Allaah kwake hatoweza kuikidhi (kuilipa funga) –ya siku hiyo aliyokula -aliyoiacha kwa kutofunga- hata kama atafunga dahari.”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf kama alivyoashiria Al-Bukhaariyy na Shaykh Al-Albaaniy amesema Dhwa’iyf  kwenye Mishkaat Al-Maswaabiyh.من اعتكف عشراً في رمضان كان كحجتين وعمرتين

حديث موضوع، ذكره الشيخ الألباني في السلسلة الضعيفة،وضعيف الترغيب والترهيب، وضعيف الجامع الصغير.ويغني عنه ماورد في الصحيح من فضل الاعتكاف في رمضان وخاصة العشر الأواخر منه.

“Mwenye kukaa I’itikaaf -siku- kumi katika Ramadhwaan huwa –jazaa yake- kama aliyefanya Hijjah mbili na ‘Umrah mbili.”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na Dhwa’iyf At-Targhiyb wat-Tarhiyb na Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.

Hakuna haja ya Hadiyth hii kwa kuwa Hadiyth zilizopokewa kwenye –vitabu- Swahiyh kuhusiana na fadhila za I’tikaaf katika mwezi wa Ramadhwaan na hasa kwenye kumi la mwisho wake zinatosheleza.كان يصلي في شهر رمضان في غير جماعة بعشرين ركعة والوتر

وهو حديث موضوع كما ذكر الشيخ الألباني في السلسلة الضعيفة، وهو خلاف حديث عائشة رضي الله عنها في الصحيحين: ما كان النبي صلى الله عليه وسلم يزيد في رمضان ولا في غيره على إحدى عشرة ركعة.

“Alikuwa -Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- akiswali kwenye mwezi wa Ramadhwaan si katika Jamaa’ah (akiswali pekee) rakaa ishirini na witr.”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah nayo ni kinyume na Hadiyth ya Ummul-Mu-uminiyna ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) iliyo kwenye Swahiyh mbili (Al-Bukhaariy na Muslim) ambayo ni:"Hakuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akizidisha si katika (mwezi wa) Ramadhwaan na wala si katika (miezi) mingine isiyokuwa -Ramadhwaan- zaidi ya rakaa kumi na moja.” [17]شهر رمضان معلَّق بين السماء والأرض، ولا يرفع إلى الله إلا بزكاة الفطر

"العلل المتناهية" لابن الجوزي، "الضعيفة" للألباني

“Mwezi wa Ramadhwaan huning’inia baina ya mbingu na ardhi, na wala hainyanyuliwi kwa Allaah mpaka kwa Zakaah ya Fitwr.”

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na Ibn Al-Jawziy katika kitabu Al-‘Ilal Al-Mutanaahiyyah."لو أن الله عز وجل أذن للسماوات والأرض أن تتكلم لبشرت الذي يصوم شهر رمضان بالجنة"

موضوع، ذكره السيوطي في اللآلئ المصنوعة.

“Lau Allaah Angeliidhinisha mbingu na ardhi kusema, basi –kama zingeliidhinishwa kusema- zingelimbashiria Jannah yule anayefunga mwezi wa Ramadhwaan.”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja As-Suyuutwiy kwenye Al-Laaali Al-Maswnuw’ah.أتاكم رمضان، شهر بركة، يغشاكم الله فيه، فينزل الرحمة، ويحط الخطايا ويستجيب فيه الدعاء، وينظر الله تعالى إلى تنافسكم فيه، ويباهي بكم ملائكته، فأروا الله من أنفسكم خيرا،
فإن الشقي من حرم فيه رحمة الله عز وجل

قال الألباني موضوع في تعليقه الترغيب والترهيب

“Mmejiwa na –mwezi wa- Ramadhwaan, mwezi wa baraka, ambao ndani yake Allaah Huwakinga nyinyi, Huteremsha Rahmah Yake, na Husamehe makosa, na Hajibu ndani yake du’aa, na Huangalia ndani yake katika kushindana kwenu –katika ufanyaji wa mema- na Hujigamba mbele ya Malaika Wake, basi muonyesheni Allaah kutokana na nafsi zenu katika yale yaliyo mazuri, kwa sababu Ash-Shaqiyu (muovu) -miongoni mwenu ni- yule aliyenyimwa Rahmah za Allaah.”Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika At-Targhiyb wat-Tarhiyb.إن الجنة لتزين لرمضان من رأس الحول إلى الحول، فإذا كان أول يوم من رمضان هبّت ريحٌ من تحت العرش، فصفّقت ورق الجنة، فتنظر الحور العين إلى ذلك فيقلن: يا رب اجعل لنا من عبادك في هذا الشهر أزواجاً تقرُّ أعيننا بهم، وتقرّ أعينهم بنا، فما من عبد يصوم يوماً من رمضان إلا زُوّج زوجةً من الحور العين في خيمة من درة مما نعت الله: {حور مقصورات في الخيام} (الرحمن :72)، على كل امرأةٍ سبعون حُلّة ليس منها حلّة على لون الأخرى، تُعطى سبعين لوناً من الطيب ليس منه لونٌ على ريح الآخر، لكل امرأة منهن سبعون ألف وصيفة لحاجتها، وسبعون ألف وصيف، مع كل وصيف صحفةٍ من ذهب، فيها لون طعام تجد لآخر لقمة منها لذة لا تجد لأوله، لكل امرأة منهن سبعون سريراً من ياقوتة حمراء، على كل سرير سبعون فراشاً بطائنها من إستبرق، فوق كل فراش سبعون أريكة، ويُعطى زوجها مثل ذلك على سرير من ياقوت أحمر موشحٍ بالدرّ، عليه سواران من ذهب. هذا بكل يوم صامه من رمضان سوى ما عمل من الحسنات

 ذكره الشوكاني في "الفوائد المجموعة في الأحاديث الموضوعة"Hakika Jannah hupambwa kwa ajili ya Ramadhwaan kila mwaka, basi inapokuwa siku ya kwanza katika (mwezi wa) Ramadhwaan huvuma upepo chini ya ‘Arsh, majani ya Jannah yakatua mahali pake, na Huwr Al-‘Ayn hutazama hayo na husema: Ee Mola! Tujaalie kutokana na waja Wako kwenye mwezi huu waume ambao macho yetu yaliwazike nao na macho yao yaliwazike nasi, basi hakuna mja atakayefunga siku katika (mwezi wa) Ramadhwaan isipokuwa ataoa mke kutokana na Al-Huwr Al-‘Ayn kwenye hema la lulu. {{Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema}} [Ar-Rahmaan: 72]…

Haya ni kwa –ajili ya- kila siku aliyoifunga katika -siku za- Ramadhwaan ukitoa yale mema aliyoyafanya.”

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ –ya kutungwa, amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Ash-Shawkaaniy katika Al-Fawaaid Al-Majmuw’ah fiy Al-Ahaadiyth Al-Mawdhwuw’ah.Ndugu yangu katika iymaan, hizo ni baadhi ya Hadiyth zilizozagaa katika jamii yetu na katika ndimi za baadhi ya wahadhiri wetu, kama tulivyoziona zote ni hatari kwa jamii na ummah kwa ujumla kama hazitoanikwa na kuwekwa hadharani kwa lengo la kumfunua macho kila mwenye kutaka kufunua macho yake na ili aangamie yule wa kuangamia kwa dalili dhahiri na ahuike mwenye kuhuika kwa dalili dhahiri.Ndugu yangu katika iymaan, kwa kumalizia waraka wangu ningependelea pia kuzitaja Hadiyth nyingine ambazo ni hatari kubwa kwa ummah kwani ziko baina ya Dhwa’iyf, na Mawdhwuw’, na Matruwkah, na Munkarah; kama hizi:

الصَّائم في عبادة من حين يصبح إلى أن يمسي ما لم يغتب؛ فإذا اغتاب خرق صومه.

“Mwenye kufunga huwa yuko kwenye ‘ibaadah kuanzia anapopambazukia mpaka anapoingia usiku madhali hajasengenya; akisengenya tu huharibika Swawm yake.”

الصَّائم في عبادةٍ من حين يصبح إلى أن يمسي، إذا قام قام، وإذا صلَّى صلَّى، وإذا نام نام، وإذا أحدث أحدث، ما لم يغتب؛ فإذا اغتاب خرق صومه.“Mwenye kufunga huwa yuko kwenye ‘ibaadah kuanzia anapopambazukia mpaka anapoingia usiku, akisimama husimama, na akiswali huswali, na akilala hulala…”اتَّقوا شهر رمضان، فإنَّ الحسنات تضاعف فيه، وكذلك السَّيئات.

“Uogopeni mwezi wa Ramadhwaan, kwani ‘amali njema huzidishwa maradufu ndani yake, na ndio hivyo hivyo kwa ‘amali mbaya.”إذا كان أوَّل ليلةٍ من رمضان، فتحت أبواب السَّماء، فلا يغلق منها باب؛ حتى يكون آخر ليلةٍ من رمضان، وليس عبد مؤمن يصلي في ليلة فيها، إلَّا كتب الله له ألفًا وخمسمائة حسنة بكل سجدة، وبني له بيتًا في الجنَّة من ياقوتةٍ حمراء، لها ستون ألف بابٍ، لكل منها قصر من ذهبٍ موشحٍ بياقوتةٍ حمراء، فإذا صام أول يوم من رمضان، غفر له ما تقدم من ذنبه، إلى ذلك اليوم من شهر رمضان، واستغفر له كل يومٍ سبعون ألف ملكٍ، من صلاة الغداة، إلى أن توارى بالحجاب، وكان له بكل سجدة يسجدها في شهر رمضان بليل أو نهار، شجرة يسير الراكب في ظلها خمسمائة عامٍ.

“Inapokuwa usiku wa kwanza katika (mwezi wa) Ramadhwaan, hufunguliwa milango ya mbingu, haufungu katika hiyo mlango wowote ule mpaka inapokuwa usiku wa mwisho katika (mwezi wa) Ramadhwaan, na haswali mja Mu-umin yeyote yule katika usiku wowote ule ndani yake isipokuwa Allaah Humuandikia kwa kila sajdah –thawabu ya- mema elfu na mia tano, na Humjengea nyumba katika Jannah…”من صلَّى في آخر جمعةٍ من رمضان الخمس الصلوات المفروضة في اليوم والليلة، قضت عنه ما أخل به من صلاة سنته.

“Mwenye kuswali katika (siku ya) Ijumaa ya mwisho kwenye (mwezi wa) Ramadhwaan Swalah tano za fardhi katika mchana na usiku - Swalah tano pekee-zitamkidhia Swalah zake zote asizoswali za mwaka wake.”من فاتته فرائض ولم يعلم عددها؛ فليصلِّ أربع ركعاتٍ أوَّل جمعةٍ في شعبان، فإن لم يتيسر له ففي أولِّ جمعةٍ من رمضان.

“Mwenye kupitwa na (Swalah za) fardhi na akawa haelewi idadi yake –hizo Swalah za fardhi asizoziswali- basi na aswali rakaa nne (kwenye siku ya) Ijumaa ya kwanza katika (mwezi wa) Sha’abaan, na kama haitokuwa wepesi kwake, basi –na aziswali hizo rakaa nne kwenye siku ya- Ijumaa ya kwanza katika –mwezi wa- Ramadhwaan.”من قضى صلاةً من الفرائض في آخر جمعةٍ من شهر رمضان، كان ذلك جابرًا لكلِّ صلاةٍ فاتت في عمره إلى سبعين سنةٍ.“Mwenye kulipa Swalah –yoyote ile- katika (Swalah za) fardhi katika Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Ramadhwaan, itakuwa ni yenye kitulizo (kisawazishi) kwa kila Swalah zilizompita katika umri wake mpaka miaka sabini.”فضل شهر رجب على الشُّهور، كفضل القرآن على سائر الكلام، وفضل شهر شعبان على الشُّهور، كفضلي على سائر الأنبياء، وفضل شهر رمضان كفضل الله على سائر العباد.

“Ubora wa mwezi wa Rajab kwa miezi mingine ni kama ubora wa Qur-aan kwa maneno mengine, na ubora wa mwezi wa Sha’abaan kwa miezi mingine ni kama ubora wangu kwa Mitume wengine, na ubora wa mwezi wa Ramadhwaan ni kama ubora Allaah kwa viumbe.”رمضان بالمدينة خيرٌ من رمضان فيما سواه.

“Ramadhwaan (kwenye mji wa) Madiynah ni bora kuliko kwenye mji mwengine wowote usiokuwa Madiynah.”رمضان بمكة أفضل من ألف رمضان بغير مكة.

“Ramadhwaan (kwenye mji wa) Makkah ni bora kuliko kwenye mji mwengine wowote usiokuwa Makkah.”والَّذي بعثني بالحقِّ نبيًا: إنَّ جبريل أخبرني عن إسرافيل عن الله عزَّ وجلَّ: أنَّ من صلَّى ليلة الفطر مائة ركعةٍ, يقرأ في كلِّ ركعةٍ الحمد لله مرةً, وقل هو الله أحدٌ عشر مراتٍ, ويقول في ركوعه وسجوده عشر مراتٍ: سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر. فإذا فرغ من صلاته استغفر مائة مرةٍ, ثمَّ يسجد, ثمَّ يقول: يا حيُّ يا قيُّوم يا ذا الجلال والإكرام, يا رحمن الدنيا والآخرة ورحيمهما, يا أرحم الرَّاحمين, يا إله الأولين والآخرين, اغفر لي ذنوبي, وتقبل صومي وصلاتي, والَّذي بعثني بالحقِّ لا يرفع رأسه من السُّجود, حتى يغفر الله له ويتقبل منه شهر رمضان.

“Naapa kwa Yule Aliyenituma kwa haki (nikiwa ni) Nabii: kwamba Jibriyl ameniambia –kuwa amepokea kutoka kwa – Israafiyl –nae amepokea kutoka kwa- Allaah kuwa: Atakayeswali usiku wa Fitwr (usiku wa ‘Iyd) rakaa mia kwa kusoma katika kila rakaa Al-Hamdu LiLLaahi mara moja, na Qul Huwa Allaah mara kumi na moja, na kusema katika rukuu yake na sujudu yake: Subhaana Allaah wal Hamdu LiLLaahi wala ilaaha ila Allaah wa Allaahu Akbar…; naapa kwa Yule Aliyenituma kwa haki hatonyanyua kichwa chake kutoka kwenye sujudu mpaka Allaah Amghufulie na Amtakabalie mwezi wa Ramadhwaan.”Ndugu yangu katika iymaan, hizo ni baadhi ya Hadiyth zisizokuwa sahihi kuhusu mwezi wa Ramadhwaan na kama tunavyoziona ziko wazi kuwa ni za kutunga na kuzuliwa uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); hivyo kama tunataka Ramadhwaan yetu iwe kweli Ramadhwaan na Swawm yetu iwe kweli ni Swawm na Qiyaam chetu kiwe kweli Qiyaam basi yaliyothibi kwenye Hadiyth Swahiyh yanatosheleza na tujitosheleze nayo. Ama yale yote ambayo hayakuthibiti kuwa ni Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa ‘aalihi wa sallam) basi ni bora na ni kheri kwetu na ndio kutakabaliwa kwa ‘amali zetu kama tutajiepusha nayo.Hivyo, ni vyema kwa kila anayepata nafasi ya kutuwaidhi asiyatumie, hata kama matamshi yake yanaonekana au yana harufu ya yale yote yenye muelekeo na Uislamu, lakini sio Hadiyth ya Mtumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na kama Hadiyth basi sio sahihi, na kuzitumia kama ni Hadiyth kwa kusema: “Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):...” hayo, baada ya kuthibiti kuwa sio sahihi, huwa ni kumzulia uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na makemeo ya kuzua uongo tunayaelewa vyema, wachilia mbali kumzulia uongo aliyeletwa kwa lengo la kuigwa.Ndugu yangu katika iymaan, tumuombe Ar-Rahmaan Atuwafikishe katika Ramadhwaan, tumuombe Atuwafikishe katika kuishi na kukaa na Ramadhwaan kwa kuifunga, kutekeleza Ayapendayo na Ayatakayo Muumba, na kuachana na makatazo Yake, pia tumuombe Muumba Atupe uwezo wa kufikisha amana kama alivyoifikisha Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Atutie mapenzi baina yetu, mapenzi yatayotupelekea kuwa tayari kusameheyana, kuhurumiana, kuvumiliana, kuheshimiana na kukosoana na kurekebishana kwa njia na namna alivyokuwa akiwarekebisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘Anhum).

[1] Aal ‘Imraan 3:102.

[2] An Nisaa 4:1.

[3] Al Ahzaab 33:70-71.

[4] Ni Hadiyth iliyokosa masharti ya Hadiyth Sahihi na ya Hadiyth Hasan.

[5] Ni Hadiyth aliyosingiziwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); Hadiyth ya uongo.

[6] Ni Hadiyth ambayo katika isnadi yake kuna raawi mwenye kutuhumiwa kuwa ni muongo.

[7] Ni Hadiyth ambayo katika isnadi yake kuna raawi aliyepindukia mipaka katika makosa yake au amekithiri katika kusahau kwake au imedhihiri ufuska wake au ni Hadiyth iliyopokewa na dhaifu yenye kwenda kinyume na yaliyopokewa na wenye kutegemewa.

[8] Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Elimu, ‘Mlango wa dhambi za mwenye kumzulia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)’.

[9] Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Elimu, ‘Mlango wa dhambi za mwenye kumzulia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)’; na Muslim, katika ‘Mlango wa Kujihadhari kutokana na kumzulia uongo Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)’.

[10] Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Elimu, ‘Mlango wa dhambi za mwenye kumzulia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)’.

[11] Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Janaazah, ‘Mlango yale yenye kuchukiza katika kumlilia maiti kwa kupiga makelele’.

[12] Mustwalahul-Hadiyth: Ni elimu ambayo hujulikana hali ya mpokezi wa Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Hadiyth yenyewe kwa kuzingatia kukubaliwa au kukataliwa kwake.

[13] Imepokelewa na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Elimu, ‘Mlango wa yaliyokuja katika mwenye kupokea Hadiyth hali kuwa anaona...’; Amesema At-Tirmidhiy: Hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh.

[14] Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Swawm, ‘Mlango wa kuharakisha kufungua kinywa; na Muslim, katika Kitabu cha Swawm, ‘Mlango wa fadhila za Suhuwr na kutiliwa nguvu kupendeza kwake’.

[15] Imepokelewa na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha sifa za Jannah, ‘Mlango yaliyokuwa katika sifa za Jannah na naimi zake’.

[16] Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Swalah ya Taraawiyh, ‘Mlango wa ‘amali kwenye kumi la mwisho la Ramadhwaan’.

[17] Imepokelewa na Al-Bukhaariyy, katika Kitabu cha Swalah ya Taraawiyh, ‘Mlango wa fadhila za mwenye kusimama Ramadhwaan’.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only