May 15, 2018

Jinsi ya kupika Sheer Khurma (Pakistani) Tambi Za Maziwa

Vipimo:
Tambi nyembamba sana (Roasted Vermicelli) - 200 gm
(Za brown tayari zimeshachomwa (roasted))
Samli -  3 vijiko vya supu
Maziwa - 7 gilasi             
Sukari - 1 kikombe
Siagi -  2 Vijiko vya supu
Njugu za Pistachio (zilizokatwa ndogo ndogo) -   ½ Kikombe
Lozi (Zilizomenywa na kukatwa ndogo ndogo) -  ½ Kikombe
Zabibu kavu -  ½  Kikombe
Hiliki  - ½ kijiko cha chai
Vanilla - 2 kijiko cha chai 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Zikatekate tambi na zikaange kidogo tu kwa  samli.  
  2. Tia maziwa gilasi 5   kwanza
  3. Tia sukari, pistachio, lozi, zabibu, hiliki na vanilla.
  4. Wacha ichemke kidogo tu kisha epua wacha ipowe.
  5. Ukumbusho: Hazitaki kupikwa sana kwani zinawiva mara moja tu.
  6. Ikishapowa tia siagi na maziwa  gilasi 2 yalio baridi sana koroga vizuri
  7. Mimina katika bakuli kisha pambia juu yake lozi nyingine kidogo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only