May 27, 2018

Kona ya waislamu wapya

SWALI:
Assalam aleikum warahma tullahi wabarakatu,
Ni nini natakiwa kufanya ili niwe muislamu?... kwasababu nina ninaniya ya kuingia kwenye uislamu ila sina uhakika wa taratibu ya kusilimu ili niwe muislamu. 
JIBU:Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihiwa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.Kusilimu mtu ni jambo jepesi kabisa ila baada ya kumsilimu kuna ya muhimu ya kuzingatia ambayo tunakuwekea maelezo chini ya hizi taratibu za kumsilimu.


Kwanza kabisa kama utaweza kumpata mwenye kujua Dini ni bora kwani ataweza pia kukuongoza na kukupa mawaidha na maelekezo muhimu baada ya kumsilimu. Ama ikiwa hayupo mwenye kuijua Dini vizuri, basi hata wewe unaweza kumslimu kwa kutekeleza yafuatayo:

  1. Utatamka utakiri Shahaada kwa kutamka wewe maneno haya kidogo kidogo au yote kwa mara moja kama utaweza, kwanza kwa Kiarabu kisha kwa Kiswahili.

Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, wa ashhadu anna Muhammadar Rasuulu-Allaah.
  
(Nakiri na kutamka kuwa hapana apasaye kwa dhati kuabudiwa ila Allaah, na nakiri kuwa Muhammad ni Mjumbe Wake)

(Haya tuliyopigia mstari unaweza kutamke ingawa si lazima sana, hutumika ikiwa mtu alikuwa Mkiristo na anaamini kuwa 'Iysa (Jesus) ni mungu au mwana wa mungu).


 Wa ash-hadu anna ‘Iysa Rasuulu-Allaah  
(Na nakiri kuwa 'Iysa (Yesu) ni Mjumbe wa Allaah na si mungu au mwana wa mungu.'

Ukitamka yote hayo hapo juu basi tayari ameshakuwa Muislamu.

  1. Ikiwa ni mwanamke Kata kucha zako, punguza au nyoa nywele za kwapani na sehemu zake za siri.  

  1. Ikiwa ni mwanaumekata kucha zako, punguza au nyoa nywele za kwapani na sehemu zako za siri, nyoa nywele za kichwani na kisha baadaye ukatahiriwe (Jando) kama bado hujatahiriwa (si lazima siku hiyo hiyo),  kutahiri ni Sunnah ya Mitume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) kama ilivyo dalili katika Hadiyth ifuatayo:

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) alimuamrisha Kafiri mwanamume aliyesilimu: ((Nyoa nywele za ukafiri na fanya tohara [jando])). [Abu Daawuud, na imepewa daraja ya Hasan na Shaykh Al-Albaaniy]

Tanbihi: Nywele za kwapani na sehemu za siri zisikae zaidi ya siku arubaini bila ya kunyolewa au kupunguzwa kwa Waislamu wote.

  1. Kuoga (ghusul) na kuvaa nguo safi kwa maana zisizokuwa na najsi yoyote kama mkojo, kinyaa au mate ya mbwa.

  1. Jifunzwe kuswali, na utekeleze Swalaah tano bila ya kuziacha

  1. Unaweza ukachagua jina lolote zuri la Kiislam ukalitumia badala ya jina lako la Kikafiri (ingawa si lazima ubadili jina lake, ila ni vizuri ili utambulike kuwa ni Muislam). Majina mazuri ni haya hapa:

    Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto

Mambo muhimu kutekeleza baada ya kumsilimu Muislamu
 

baada ya hapo, Tafuta vitabu vya Dini, Jifundishe Dini vizuri, mtafute Mwalimu aweze kukufundisha Uislam. Makosa makubwa yanafanywa sana na Waislam, ni kuwa baada ya kumsilimisha mtu humwacha akaenda zake na hawamfuatilizii wala hawamsaidii kumfundisha Dini wala kujua kama anaswali, anafunga n.k. Jaribu kumsaidia kwa hali na mali kadiri uwezavyo ili kumpa moyo na kumuonyesha undugu wa Kiislamu.

kwa msaada zaidi wasiliana nasi katika coment au kwa email yetu Uislamuwangu@gmail.com au muislamublog@gmail.com nasi tutakusaidia kadri tutakavyojaalia.Na Allaah Anajua zaidi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only