August 19, 2018

Tunawakumbusha Kutamka Du’aa Bora Kabisa Siku ‘Arafah Pamoja Na Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi!

Tunawakumbusha Kutamka Du’aa Bora Kabisa Siku ‘Arafah
Pamoja Na Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi,
Kuomba Maghfirah Na Kumuomba Allaah Haja Zako Akutaqabalie.Kwanza: Inapoingia Alfajiri ya Siku ya ‘Arafah, inapasa kutamka kwa wingi du’aa ifuatayo ambayo ni maneno bora kabisa aliyoyatamka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Manabii kabla yake kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي
“Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:

Laa Ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku Walahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr. [At-Tirmidhiy]

Hapana mwabudiwa wa haki  ila Allaah, Pekee, Hana mshirika, Ufalme ni Wake, na Himdi zote ni Zake Naye juu ya kila kitu ni Muweza.

Pili:  Siku ya ‘Arafah ni Siku ambayo Allaah ('Azza wa Jalla) Huteremka duniani kwa uteremko unaolingana na Utukufu Wake na kuwaacha huru kwa wingi waja Wake kutokana na Moto kwa dalili:

 عنْ عَائِشَةَ أنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "‏مَا مِنْ يَوْمٍ أَكْثَرَ مِنْ أَنْ يُعْتِقَ اللَّهُ فِيهِ عَبْدًا مِنَ النَّارِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ وَإِنَّهُ لَيَدْنُو ثُمَّ يُبَاهِي بِهِمُ الْمَلاَئِكَةَ فَيَقُولُ مَا أَرَادَ هَؤُلاَءِ"‏‏.‏
Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambayo Allaah Anayoacha kwa wingi huru waja kutokana na moto kama siku ya ‘Arafah.  Na huwa karibu kisha Anajigamba kwao kwa Malaika na Husema: Wametaka nini hawa? [Muslim]

Na katika Riwaayah nyingine:
اشْهَدُوا مَلاَئِكَتِي أَنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ. صحيح الترغيب
Shuhudieni Malaika wangu kwamba hakika Mimi Nimewaghufuria)) [Swahiyh At-Targhiyb (1154)]

Kwa hiyo omba maghfirah na mdhukuru Allaah ('Azza wa Jalla) kwa wingi kabisa, na muombe Allaah du'aa zako Akutaqabalie Siku hii tukufu kwa aliyejaaliwa Hajj au asiyejaaliwa kwenda Hajj.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only