August 10, 2018

Ukumbusho Wa Takbiyrah Katika Masiku Kumi Na Tatu Ya Dhul-Hijjah: Tarehe 1–13 Dhul-Hijjah

Ndugu Waislamu! Tukumbushane kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyrah  kuanzia unapoandama mwezi wa Dhul-Hijjah mpaka mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani kuanzia tarehe 1 Dhul-Hijjah mpaka 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake. Hivi ni kutokana na amri dalili zifuatazo. Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:


لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ
 ((Ili washuhudie manufaa yao; na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu kwa yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo.    [Al-Hajj  28]

Na pia:

كَانَ إبْن عَمَر وَأبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّه عَنْهُما يَخْرُجَانِ إِلَى السُّوقِ فِي أَيَّامِ العَشْرِ يُكَبِّرَانِ، وَيُكَبِّرُ النَّاسُ بِتَكْبِيرِهِمَا .
Ibn 'Umar na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walikuwa wakienda sokoni katika siku kumi (za Dhul-Hijjah) na kutamka Takbiyr kwa sauti na watu wakiwaigiza. [Al-Bukhaariy]

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ
Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika.  [Al-Baqarah: 203]

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku maalumu ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah[Al-Qurtwubiy: 3.3]

Inavyopasa kufanya Takbiyrah:

   اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ،  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd


Inapasa kuwakumbusha ndugu wengine mafunzo haya na kuwasisitiza ili kila mmoja apate thawabu za kufufua Sunnah hizi ambazo wengi wamegafilika nazo.
Thawabu hizo zitazidi kuongezeka kwa yule atakayeanza kumfundisha mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kufundishwa: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ .
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Atakayetenda kitendo kizuri (Sunnatun-Hasanah) katika Uislaam kisha nacho kikafuatwa kutendwa, ataandikiwa mfano wa ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao.”  [Muslim]Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only