Al-Lajnah Ad-Daa'imah: Hairuhusiwi Kupongezana Kwa Mnasaba Wa Mwaka Mpya Wa Hijri (Kiislamu)

Hairuhusiwi Kupongezana Kwa Mnasaba Wa Mwaka Mpya Wa Hijri (Kiislamu)

Al-Lajnah Ad-DaaimahSWALI:

Je, inaruhusiwa kuwapongeza wasio Waislamu kwa mwaka mpya wa kwao wa Gregori.
Na je, kupongezana kwa mwaka wa Kiislamu wa Hijri, na je, kupongezana kwa (sherehe ya) Mawlid?


JIBU:

Hairuhusiwi kupongezana kwa minasaba hiyo yote, kwa sababu haijawekewa shariy'ah kusherehekea (masiku hayo).

Tunamuomba Allaah At-Tawfiyq, na Swalaah na Salaam zimwendee Rasuli wetu Muhammad, familia yake na Maswahaba zake.


[Al-Lajnat Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Wal-Ifta, Fatwa namba 20795]

0 Comments