Mema Yaliyobakia الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ Ni Bora Kuliko Mali Na Watoto

Mema Yaliyobakia الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ Ni Bora Kuliko Mali Na WatotoAnasema Allaah سبحانه وتعالى:

 الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾
46. Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Rabb wako, kwa thawabu na matumaini.  [Al-Kahf: 46]

Allaah Ametutajia mapambo ya dunia katika Aaayah hii tukufu, lakini baada ya kuyataja hayo mapambo katukumbusha kuwa mema yanayobakia - َالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ ni bora zaidi kuliko mali na wana. 

Ndugu Muislamu jiulize basi: 

1-Kwa nini mapambo hayo sio bora kuliko mema yanayobakia?       الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ  
2-Nini maana yake  mema yanayobakia?َالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ     

 Bila ya shaka sote tunayapenda mapambo hayo ya dunia. Na sio hayo tu bali mengi zaidi ya hayo kama Alivyoyataja Allaah سبحانه وتعالى katika aya hii nyingine:

 زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾
14. Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri. [Aal-‘Imraan: 14]

Hata hivyo baada ya kutaja mapambo hayo mengine, Ameendelea Allaah سبحانه وتعالى kutukumbusha tena kwa kutuuliza swali!
قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾
15. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na wake waliotakasika na radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja. [Aal-‘Imraan: 15]

Kama tunavyoona kuwa yaliyo bora zaidi ya mapambo ya dunia ni Pepo ya Milele na zaidi baada ya kupata Pepo ni kupata Radhi Yake Allaah سبحانه وتعالى.

Vile vile kuna hatari yake hayo mapambo kwani huenda wakati mwengine yakawa ni mtihani au adui yetu kama Alivyosema katika aya hizi:

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٤﴾
14. Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [At-Taghaabun: 14]

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿١٥﴾
15. Hakika mali zenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Allaah kuna ujira adhimu. [At-Taghaabun: 15]

Huenda mapambo hayo yakawa adui yetu au majaribio kwani yakasababisha tukayapenda sana hadi yakatupeleka kufanya yasiyomridhisha Allaah سبحانه وتعالى , au yakatughafilisha na kumkumbuka Allaah سبحانه وتعالى , na yakatusahaulisha kabisa na Akhera hadi mauti yatakapotufikia, na mwishowe tukawa ni wenye khasara kubwa kama Alivyosema Allaah سبحانه وتعالى
 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Zisikupurukusheni mali zenu na wala watoto wenu mkaacha kumdhukuru Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo basi hao ndio waliokhasirika. [Al-Munaafiquun: 9]

Ama  mema yanayobakia - الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ haya ndio yatakayotupatia faida kwani hutangulia mapema kuwekwa Akhera yakawa kama hazina ambazo tutazikuta tutakaposimama mbele ya Mola Mtukufu kuhesabiwa siku ya Qiyaamah.

Ibn 'Abbaas,  amesema kwamba  mema yanayobakia - َالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ ni kusema:

سُبْحَانَ اللهِ،  الحَمْدُ لله ِ,   لاَ إِلَهَ إلاَّ الله ُ, اللهُ أَكْبَر,  لاَ حَوٍلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ بالله ,  تبَارَكَ اللَّه, أَسْتَغْفِرُ اللَّه

Subhana-Allaah, ِAlhamduli-LLaah, Laa Ilaaha Illa Allaah, Allaahu Akbar, Laa Hawlah Wa Laa Quwwata Illa BiLLaah, Tabaraaka Allaah, Astaghfiru-LLaah.


Vile vile kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم, Swalah tano za kila siku, Hajj, Swaum, Zakaat, Sadaqah, Kuachia huru watumwa, Jihaad, kuungana na ndugu na Jamaa, na vitendo vyote vyema.

عن ثوبان رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((بخ ٍ بخٍ لخمس ما أثقلهن في الميزان : لا إله إلا الله ، وسبحان الله ، والحمد لله ، والله أكبر، والولد الصالح يتوفى للمرء المسلم فيحتسبه)) النسائي وابن حبان والحاكم ، وأحمد ، وصححه الألباني في صحيح الجامع    

Imetoka kwa Thuubaan رضي الله عنه ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلمamesema: ((Heko heko kwa vitu vitano, uzito gani vitakavyokuwa  katika Mizani; Laa Ilaah Illa- Allaah, Wa-Allaahu Akbar, Wa Subhaanah-Allaah, Wa-AlhamduliLLah, na mtoto mwema atakayekufa na wazazi wake wanatarajia thawabu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)) [An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Ahmad, na kaisahihisha Al-Albaaniy katika 'Swahiyh Al-Jaami']

Kwa hiyo tambua ndugu Muislamu kuwa maskini asiyemiliki nyumba wala mali yoyote wala kitu chochote, lakini amechuma mema yanayobakia - َالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ japo kutaja hizo tasbiyh pekee ni bora mbele ya Allaah kuliko tajiri mwenye kumiliki mali nyingi lakini hana mema yanayobakia -َالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ

Hii ni miongoni mwa Neema na Rahma za Mola Muumba na Uadilifu Wake kwa waja Zake.

0 Comments