October 9, 2018

Al-Lajnah Ad-Daa'imah: Hukmu Ya Aliyefariki Kuitwa "Marehemu"

SWALI:

Baadhi ya watu pindi anapofariki mtu, husema: “Amefariki fulani Al-Marhuwm” (Marehemu) au husema: “Amefariki fulani Al-Maghfuwr Lah” (Ameghufuriwa) na kauli kama hizo; je, inajuzu? Na nini hukmu yake?


JIBU:

Linalopasa zaidi ni kumtaja maiti aliye Muislamu kwa kusema: Rahimahu-Allaah (Allaah Amrehemu) au Ghafara Allaahu lah (Allaah Amghufurie) kwa kuwa ni du’aa kwake kumuombea maghfirah na rahmah. Na hii ndio inakubalika, lakini si kusema “Al-Marhuwm” (Marehemu - karehemewa) au “Al-Maghfuwru lah” (Ameghufuriwa) kwa sababu hivi ni kama kukata maamuzi (kuthibitisha) kuwa ameshaghufuriwa au amesharehemewa, na hali sisi hatuthibitishi hivyo kwa yeyote isipokuwa kwa dalili kutoka Kitaabu na Sunnah.

Wa biLLaahi At-Tawfiyq.
Swalaah na salaam kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba zake.

[Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-‘Ilimiyyah, Swali Namba (21121)]


Tanbihi:
Kuna Wanachuoni kama Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) wanaoona inafaa kumuita maiti "Marehemu", lakini kauli yenye nguvu ni hiyo juu ya Al-Lajnatud-Daaimah.
Wa Allaahu A'lam.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only