October 6, 2018

Imaam Sufyaan Bin Ath-Thawriy: Nasaha Muhimu

Imenukuliwa kutoka: Maisha ya Sufyaan ath-Thawriy, ukurasa 176-181

Imaam Sufyaan (Allaah Amrehemu) alisema:
“Kuwa mkweli wakati wote na kila mahali. Jiweke mbali na uongo na udanganyifu, na usikae pamoja na watu waongo na wadanganyifu, kwa kufanya matendo yote haya ni madhambi makubwa.
Ndugu yangu, jihadhari na usijionyeshe aidha katika khutbah au matendo yako, kwa sababu kujionyesha ni jambo la Shirki (Shirki – ni kumfanya Allaah kuwa na mshirika katika ibada yoyote ile).
Usiwe ni mwenye kujiona, hata ikiwa ni kwa tendo zuri kumbuka kuwa halitopanda mbinguni kama tendo hilo litakuwa na majivuno yoyote ndani yake.
Chukua dini yako kutoka tu kwa yule ambaye (ni mwangalifu na) mwenye dhati na huruma kuhusiana na uongozi wake mwenyewe kidini. Mfano wa Mwanachuoni ambaye si mwangalifu kuhusu dini yake, ni kama mfano wa daktari ambaye ni mgonjwa.
Hali kadhalika, ikiwa mtu mwenyewe hawezi kutibu ugonjwa wake, basi vipi atawezeje kutibu magonjwa ya wengine?
Kwahiyo, kama mtu si mwenye kujali na kustawisha kithabiti dini yake, vipi basi ataweza kujali juu ya dini na ustawi wa wengine?
Ndugu yangu, dini yako si kingine zaidi kuliko mwili na damu yako (yaani, unapaswa kujali dini yako vizuri, kwa sababu kama sivyo, mwili wako na damu ndivyo vitakuja kulipa fidia kwa adhabu ya Allaah). Lia juu ya wasiwasi wa nafsi yako, na kuwa ni mwenye huruma juu ya hilo. Ikiwa hutokuwa na huruma juu ya nafsi yako, basi huruma haitojionyesha juu yake.
 
Kaa tu kwenye kundi ambalo wanakunasihi. Kuwa na tamaa kidogo juu ya dunia hii na wanaokuhimiza wewe kuweka matumaini zaidi katika Akhera. Kuwa makini (muangalifu) sana kukaa na watu wa kidunia ambao huongelea mara kwa mara kuhusu masuala ya kidunia. Watu wa namna hiyo wataharibu ustawi na umakinifu wa dini yako na watachafua moyo wako.
Kumbuka kifo mara nyingi, kama jinsi unavyomuomba Allaah  mara kwa mara Akusamahe madhambi yako yaliyopita.
Muombe Allaah Akulinde salama (uovu, magonjwa ya hatari, kutokana na fitna na dhiki, n.k.) kwa ajili ya uhai wako uliyobaki.
Ndugu yangu, boresha tabia nzuri na njema. Usifanye kitendo ambacho ni kinyume na Jama'ah, kwa ajili ya wema na usalama ni matokeo ya wewe kuwa kwa amani na Jama'ah.
Yeyote mwenye kufanya juhudi daima kwa ajili ya dunia hii ni kama mfano wa mtu ambaye anajenga nyumba moja na kuharibu nyingine (kwa sababu anajenga ufanisi kwa ajili yake mwenyewe katika dunia hii, wakati yeye anaharibu bahati yake yote ya kuwa na mafanikio katika Akhera).
Toa nasaha za dhati kwa kila Muislamu ambaye anakuuliza swali kuhusiana na dini yake. Na kamwe usiwe ni mwenye kuficha ushauri mzuri kwa mtu yeyote yule ambaye anakuuliza juu ya jambo litalomuelekeza katika radhi za Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala).
Ikiwa utampenda ndugu yako (Muislamu) kwa ajili ya Allaah, basi mpatie kutoka kilichoko kwako mwenyewe na mali yako.
Jiweke mbali na mambo ya mijadala, malumbano, ugomvi, na migogoro. Kinyume chake utakuwa mgomvi (mbaya) kwa watu, utakuwa muasi na utajenga uadui na watu.
Kuwa na subira wakati wote na kila mahali, kwa kuwa uvumilivu unaongoza kwenye uadilifu na uadilifu unaongoza Peponi. Usiwe ni mwenye hasira na kununa, kwa kuwa hizo hisia mbili zinasababisha uovu, na uovu unaongoza motoni.
Usiwe mshindani na Mwanachuoni. Kwa kufanya hivyo itamfanya yeye aweze kukuchukia na hatimaye kukutenga. Kuwa na nafasi ya wewe kuwatembelea Wanavyuoni (na kujifunza kutoka kwao) kwa kuwa ni rahma kufanya hivyo.
Kinyume chake kukatana nao mbali ina maana mtu kajitwika mwenyewe ghadhabu ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala).

Bila shaka, Wanavyuoni ndiyo hazina za Manabii ('Alayhimus Salaam) na pia ndiyo warithi wao.
Jiweke mbali na anasa za ulimwengu na vitu visivyokuwa na faida, na matokeo yake Allaah Atakuwezesha kuona makosa na kasoro za dunia hii.

Kuwa mtu Wara' (ucha Mungu, na ni yule ajiepushaye na mambo yote ya shubuhaat na baadhi ya mambo ambayo ni halali kwa kuhofia tu mambo hayo yasije kumpelekea katika mambo ambayo ni haramu katika Uislamu), na (Siku ya Qiyaamah) Allaah Atafanya kikao chake cha uwajibikaji kiwe ni rahisi kwake.
Acha mambo mengi ambayo ni yenye mashaka (utata) katika dini yako, na badala yake yabadilishe kwa kufanya au kufuata mambo yasiyo na mashaka au na utata. Utaona Matokeo yake kuwa utabaki ukiwa Salama. Kwa kujiepusha na yote yenye mashaka na utata, utabaki huku ukiwa salama katika dini yako.
Amrisha wenzio kufanya mema na kataza yaliyokuwa maovu. Kwa kufanya hivyo utapendwa na Allaah. Jitenge na mabaya na pambana na Shaytwaan.

Kama unataka kuwa shujaa (wa kuikuza imani), basi kuwa mwenye furaha kiasi na cheka kidogo pindi unapopata vitu kadhaa kwenye hii dunia.

Jihusishe sana na kuitumikia Akhera, ukifanya hivyo Allaah Atakutosheleza kwa kila jambo lako linalohusiana na dunia hii (hata liwe kubwa kiasi gani).
Muombe Allaah usalama (kwenye dini yako na dunia). Ukikusudia (ukinuia) kufanya kitu kwa ajili ya Akhera yako – mathalan kama kutoa Zakaah, Swadaqah n.k. - Basi jihimize kufanya hivyo haraka kabla ya Shaytwaan hajakushawishi na usiweze tena kufanya ‘amali hiyo.

Usiwe ni mwenye kula sana (kwa kupitiliza), ambapo ukawa sasa unafanya kazi kidogo zaidi ya unavyokula. Kwa sababu hilo ni lenye kuchukiza (katika Uislamu).

Usile tu bila ya kuwa na njaa, na usile mpaka wakati utapokuwa na njaa.
Na usijaze tumbo kila wakati ukaja kuwa kama maiti, ikasababisha kutomkumbuka Allaah wakati wa uhai wako. (kwa kuwa mwenye kula kila wakati na kushiba anakuwa kishatimiza hamu/tamaa zake)
Punguza kukwaruzana na wale uliowakosea, kubali kujiweka chini na kuomba radhi (wale uliowadhulumu na kuwakosea). Vilevile msamehe kila uliyemkosea na kumdhulumu.
Kuwa mfano wa mtu ambaye watu wote kiujumla hutarajia mambo mema kutoka kwako; na mabaya (maovu) ya watu kwako iwe ni mwenye kuhisi salama tu na amani.
Kamwe usimchukie yeyote ambaye ni mwenye kumuabudu Allaah (Muislamu), na kuwa mkarimu kwa jumla watu wote na kwa wale haswa ambao wanakutegemea.
Kumbuka usije kukata mahusiano ya tumboni (yaani mahusiano na familia na jamaa). Unga mahusiano mazuri na wale ambao wamejitenga mbali nawe.
Wasamehe waliokudhulumu; utaona natija yake na utakuwa mingoni mwa Maswahaba wa Manabii na miongoni mwa Mashahidi (hiyo siku ya Qiyaamah).
Usiwe ni mwenye kufanya ziara za mara kwa mara kwa mara sokoni (madukani), kwa kuwa watu wengi huko (wauzaji na wanunuzi) ni mbwa mwitu waliovaa nguo za watu. Soko mara nyingi ndiyo maeneo ya Shaytwaan – Shaytwaan wa kibinaadamu na wa kijini. Na ikiwa kutakuwa hakuna budi ila kwenda basi ni wajibu juu yako kuamrisha mema na kukataza maovu – Lakini jua ya kuwa hutoona kingine zaidi ya maovu huko.
Simama upande mmoja wa soko na uanze kuwalingania watu:
“Ninashuhudia ya kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah peke Yake. Hana mshirika. Utawala wa mambo yote ni kwa Allaah.
Yeye ndiye Anayestahiki kusifiwa kwa haki. Yeye ndiye anayetoa uzima, na Yeye ndiye anayefisha. Mema Yote yapo katika mikono yake na ni Muweza juu ya kila jambo. Hakuna aidha uwezo wala nguvu ila ni kwa Allaah (Subhanaahu Wa Ta'ala), Mwenye nguvu.
Usiingiye katika ugomvi na watu wa dunia hii katika mambo yao ya kidunia.
Matokeo yake, Allaah Atakupenda na watu wa duniani watakupenda.
Na kuwa mnyenyekevu. Wakati uko na afya njema fanya matendo mema, utaruzukiwa usalama na afya njema (ya kimwili na utulivu wa roho) kutoka kwa Aliye juu.
Kuwa mtu mwenye kusamehe, utapata mambo yote unayotaka.

Kuwa mtu mwenye shukran, na vitu vyote (na watu) vitakuwa ni vyenye shukran kwako.
Ndugu yangu, usiruhusu (usiache) siku yako, usiku au masaa yapite huku uko kwenye mambo ya upotevu yasiyokuwa na faida. Tumia muda wako mwenyewe kwa faida yako mwenyewe - kwa ajili ya siku hiyo ya kiu (siku ya Qiyaamah).

Ndugu yangu, kiu chako hakitokatika siku hiyo ya Qiyaamah isipokuwa ikiwa Mwingi wa kurehemu kama Atakuwa radhi na wewe. Na huwezi kupata radhi zake njema siku hiyo ispokuwa ikiwa wewe ni mtiifu kwake. Fanya matendo mema yaliyokuwa mengi  kwa hiari yako mwenyewe, kwa kuwa yana athari ya kukujongeza karibu zaidi na Allaah.
Kuwa mkarimu, na makosa yako yatafunikwa, na Allaah Atakuwekea wepesi katika kikao cha uwajibikaji (hiyo siku ya Qiyaamah) pia Atakuondolea hofu.
Tenda mengi mema mno, Allaah Atakufanya uweze kuhisi furaha na kustarehe katika kaburi yako. Kaa mbali na matendo yote ya haramu, na hivyo basi utaweza kuionja ladha ya imani. Kaa katika makundi ya wachaji Mungu na watu wema, Allaah Atakufanyia vizuri mambo ya dini yako. Shikamana (tangamana) na wale wamchao Allaah. Harakisha (kuwa na pupa) ya kutenda mazuri, na Allaah Atakulinda wewe na kumkosea.
Mkumbuke Allaah mara nyingi, na matokeo yake Allaah Atakufanya uwe ni mwenye tamaa kidogo sana na hii Dunia.

Kumbuka kifo mara nyingi, na matokeo yake Allaah Atafanya mambo yako ya kidunia yawe rahisi (hata yakiwa mazito aje), na utakuwa ni mwenye kutamani tu Pepo, na matokeo yake Allaah Atakusaidia uweze kumtii kwa wingi.

Kuwa ni mwenye hofu sana na Jahannam, na matokeo yake Allaah atafanya iwe rahisi kwako uweze kusubiri matatizo yote ya maisha haya ya Duniani."

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only