October 31, 2018

Ulimwengu Wa Wamasoni (1)

Imetafsiriwa na Naaswir HaamidNamna Gani Dunia Inaendeshwa Kitaalamu?
Mnamo Ogasti ya 2, 1990 majeshi ya Saddam Hussayn yalikwaruzana na vikosi vya ulinzi vya Kuwaiti iliyo tajiri kwa mafuta kwa khofu ya Iraqi kuivamia Saudi Arabia. Marekani na majeshi yake ya ushirika yalijimwaga ndani ya eneo la Arabuni kutengeneza himaya itakayojulikana kwa jina la Ngome ya Jangwani. Hayo yalipelekea kwenye meza ya mazungumzo ya kisiasa, maelewano na majibu yake ambayo mara moja yaliporomoka na kutotarajia lolote. Mnamo Ogasti ya 17, 1991 Ngome ya Jangwani ikawa ni Jangwa la Makombora.


Migongano hiyo ilishuhudiwa na mamilioni ya watu kupitia IF, CNN na BBC zikionesha propaganda za mtindo wa kuondosha majeshi ya Saddam kwa ushirikiano wa mataifa yaliyo juu kwenye teknolojia, kisiasa na nguvu za kiuchumi. Hata hivyo, kisichoeleweka ni kwamba kuanzia muono wake wa nje, vita hivyo vilitengenezwa, kuendeshwa na kufanyiwa hila na kundi lililo werevu. Kundi ambalo limejitengeneza kiudanganyifu kama mwanaadamu aliye na nguvu juu ya mamilioni ya majeshi yaliyo na nguvu kwa hila za nuclear. Mtu ambaye amepata kushikilia 1/5 ya mafuta yote duniani kwa usiku mmoja; hata hivyo, ukweli ni kwamba hakuwa chochote isipokuwa alikuwa na duru yake kama walivyo wengine. Ni kama mfano wa kijibwa ndani ya mpango mkuu wa Vita vya Ughaibuni na pia kama ni mpigaji filimbi. Wapigaji filimbi hao wa Vita hiyo sio kwamba hawaeleweki katika kuendesha matokeo makuu Duniani. Ukweli ni kwamba wamefanya hivyo kwa kipindi kirefu, sasa ni karne.

Kuanzia kujificha kwao katika kila vita vikuu wanavyoviongoza wao, mapinduzi na mgawanyo. Wana mikono yao katika kila kitu unachosoma, kila kitu unachosikia na kila kitu unachoona. Wamefanikiwa kuingiza ndani ya kila ubongo wa mtu aina za fikra zao na kutumbukiza watu wao kwenye mamlaka za nchi zilizo muhimu na ni kutokana na kivuli hichi wamekitumilia kuanzisha mfumo mpya wa kisiasa, mfumo mpya wa kiuchumi na bila ya shaka mfumo wa dini ulio sheheni dhambi. Lengo lao la moja kwa moja ni kuhodhi mamlaka ya ulimwengu mzima na watafanya kila waliwezalo kuzuia chochote kitakachokuwa ni kikwazo kufikia malengo yao. Shabaha ambayo imewekwa wazi ndani ya risala iliyotolewa na Raisi mstaafu wa Marekani, George Bush: "Kilicho mbele yenu ni zaidi ya nchi moja ndogo, ni fikra mpya na Mfumo Mpya Wa Ulimwengu".

Hata hivyo, asili ya mpango wa ulimwengu mzima haukuanzishwa ndani ya ofisi zaWhite House. Ukweli ni kwamba, mizizi yake imeanzia kwenye vita vyengine, huko mwaka 1095 sehemu za Claremont – Ufaransa. Karne ya 11 ya Ulaya ilitawaliwa na kanisa ambalo liliwakamata barabara watu, kuanzia mioyo yao hadi fikra zao. Nguvu hii ilimuwezesha Papa Erwin II kuanza vita alivyoviita takatifu (crusade) dhidi ya Kiongozi wa Kiislamu kwa jina la Vita Vya Msalaba kuikomboa ardhi ya Jerusalem. Ardhi ambayo ilikuwa chini ya himaya ya Waislamu tokea mwaka 637, lakini mwaka 1099 himaya hii ilikhitimishwa kwa umwagaji damu na ghafla moja ikafikia tamati.Kwa jina la Msalaba, wanawake walibakwa na kuuawa, watoto walikatwa mapanga na inasemekana kwamba damu iliogelea kwenye mitaa hadi kufikia urefu wa goti la farasi. Nje ya ardhi hii ya umwagaji damu kulikuwa na kundi linalotisha (terror) ambalo litafanya lolote kupata wanalotaka hata kwa gharama yoyote. Miaka ishirini baada ya kuchukuliwa Jerusalem, Baytul-Maqdis ilitekwa nyara na kundi la wapiganaji waliookoka wanaojiita wenyewe Wapiganaji Wa Hekalu La Sulaymaan au kiufupi Wapiganaji Wa Hekalu.

Huko Jerusalem, Wapiganaji Wa Hekalu walianza kuachana na mafunzo ya Ukristo mbali zaidi na zaidi. Walijifunza siri za usanii wa Kabala na mitindo ya kale ya uchawi wa Kiyahudi pamoja na miiko yake isiyoeleweka. Mayahudi hao walijifunza usanifu wa kale wa kipagani kutoka Misri kwenye kipindi cha utumwa chini ya Firauni na kuziendeleza ndani ya Babylon katika kipindi cha utawala wa Navakanazar. Mnamo mwaka 1307, Mfalme Philip wa Ufaransa aliwatia hatiani kwa mashitaka ya kumkataa Kristo, liwati na ibada za mizimu pamoja na uchawi. Mnamo mwaka 1314, Papa Claymont V alitangaza kwamba Mahekalu yote ni ya urithi wa Ukristo na kuamrisha kwa nguvu zote majengo hayo kushikiliwa. Kiongozi wao aitwae Chekthemolay alitekwa nyara na kuchomwa.

Hekalu hilo lilizungushiwa pembe zote na karibu ya kumaliza kazi hiyo itakayodumu milele, matumaini yaliibuka lakini walihitajika kutafuta mshirika wa usalama wao lakini sio kwa Ufaransa. Walihitaji nchi ambayo ipo kwenye shauku kubwa ya kupigania uhuru dhidi ya Waingereza, nchi ya Scotland ilifaa kwa hili. Nchi ambayo matumaini yake ya uhuru yalififia kutokana na kifo cha William Wallace. Hata hivyo, kwa Mfalme wa Scotland, Robert Bruce, kuwasili kwa Wapiganaji Wa Hekalu kulimpa zana ya siri mpya. Uzoefu wao ulipatikana kwa zaidi ya miaka mia mbili ya kupigana dhidi ya majeshi makubwa ya Uislamu, mapigano ambayo yaliwafanya kuwa wataalamu katika kujihami na upiganaji kuliko mapigano yoyote ambayo yanaweza kuletwa mbele yao.
Mnamo mwaka 1314, Wapiganaji Wa Hekalu waliungana na Robert Bruce na jeshi lake lilichukuwa sehemu za Ballack Burn, wakiwa tayari kusubiri mapigano pamoja na Waingereza. Uoni wa Robert Bruce kwenye pembe zote nne ulimuwezesha kulipiga vibaya mno jeshi lenye wapiganaji 25,000 lililo na nguvu la Muingereza dhidi ya wapiganaji 6,500 tu. Ndoto ya Scotland iliyo huru hatimaye ilifikiwa. Wapiganaji Wa Hekalu sasa wamerudi na hawatakuwa tayari tena kujikubalisha kushindwa.
Wakati huu, wataiendesha nchi hiyo kwa kuwadhibiti Wafalme wake na ili kuficha siri yao moja kati ya mawili lazima
yatendeke;ama wafe Wapiganaji Wa Hekalu wote au jina lao life. Wapiganaji Wa Hekalu ambao walitoroka Ulaya, hatimaye walizikwa huko Rovelin Chapel – Scotland (kama inavyoonekana kwenye picha hapo kushoto) jengo ambalo hadi leo linasimama kama ni alama ya kuwepo kwao nchini Uingereza. Vizazi vyao vilikuja kuwa na nguvu sahihi ya Scotland. Kifo cha Malkia Elizabeth I mnamo mwaka 1603, kiliiacha Uingereza bila ya mrithi wa kiti cha ufalme. Kwa mnasaba wa kizazi cha Mfalme James V wa Scotland ndiye atakayekuwa Mfalme wa Uingereza, na kwa kufanya hivyo, Scotland na Uingereza walilazimika kujiunga pamoja kuunda utawala mpya. Na nguvu ambayo ilikuwa nayo Wapiganaji Wa Hekalu juu ya Scotland iliwaenea kuwapa himaya thabiti ya Uingereza yote. Kwa zaidi ya miaka mia moja, Wapiganaji Wa Hekalu walizificha shughuli zao chinichini hadi walipojulikana kwa uchache na kukumbukwa kidogo. Hata hivyo, hawakusimama kukamata himaya thabiti ya Uingereza.
Kipindi chote hicho walikuwa wakipanga na kujipangua na kujiingiza ndani ya uongozi katika pembe zote za utawala. Mwaka 1717, Wapiganaji Wa Hekalu walijitokeza tena Uingereza wakiwa wengi na nguvu zaidi, na sasa wakiwa tayari kujibadilisha utambulisho wao utakaokuwa mbali na sifa yao ya hapo nyuma. Hawakupata hadhi isipokuwa kwa wakuu na watawala wa Uingereza na jina walilolijichagulia lilikuwa ni jina litakalojulikana na wengi lakini litakaloeleweka na wachache. [Sikubaliani na jina la "freemasons" linalotokana na Kifaransa "frerés masons" yaani ndugu wa Kimasoni. Ni Waingereza wasioelewa ndio waliolibadilisha kuwa Freemasons].

Utambulisho huo mpya kwa wajumbe wenye mamlaka za kuamrisha mambo uliwawezesha Wamasoni kuwa na sifa na heshima. Mwanachama wa mwanzo wa Kimasoni kimataifa alikuwa ni Frederick, Mtoto wa Mfalme wa Wales.Mwanachama wa hivi karibuni ni Phillip, Mtoto wa Mfalme wa Duke wa Edinburgh na mwandani wa karibu wa Malkia wa leo wa Uingereza Bibi Elizabeth II ambaye yeye mwenyewe ni mlezi wa zamani wa Wamasoni. Hata hivyo, nyuma ya milango iliyofungwa, Wamasoni walikuwa huru kujihusisha na maadili na kanuni za siri zilizokabidhiwa kwao na wazee wao, na hizi zikaja kuwa ni msingi wa kiwango cha uwanachama kiitwacho Degree. Wamasoni hawakujihusisha tu na mfumo wa Uingereza peke yake, mawazo yao yalikuwa mbali ya hapo. Miaka inayokuja badaye, wakati ambao Dunia na Marekani zitatumbukizwa kwenye vita na mapinduzi zaidi na zaidi, mmoja kumshinda mwenziwe. Hata hivyo, hayakuwa haya ni malengo makuu yaliyokuwa yakiaminika kuwa na athari kwa wenye kuonewa. Lakini ukweli ni kwamba mipango ilibuniwa na watu wachache maalumu, waliokuwa na njaa ya uongozi katika kila kitu. Yote haya yatatokea ndani ya nchi zao walizozikimbia kwa karne zilizopita na nchi hizi zitakuwa ni msingi wa Kuutawala Ulimwengu Mzima.

Katika karne ya 18, idadi kubwa ya Wafaransa walikuwa ni masikini wakati koo za kifalme na zile zinazojiweza zikiishi kwa starehe na ubadhirifu, kukaibuka tofauti kubwa baina ya matabaka haya mawili. Wamasoni watatumia hili kushurutisha madaraka juu yao na hivyo kusababisha mgongano mkubwa katika historia ya Ufaransa. Wamasoni wakachukua nafasi hiyo ya hali mbaya iliyojaa ghadhabu miongoni mwa Wafaransa na wakatumia hilo kufanikisha malengo yao kwa kupanga vizuri vita vya propaganda. Walivihodhi vyombo vyote vya habari kisawasawa na walivitumia kuyapinda maoni ya walio wengi. Magazeti yalitezwa nguvu kutangaza mwisho wa utawala wa kifalme na kuanzisha jamii inayofuata uhuru, usawa na ushurutishwaji.

Mamilioni ya fedha yalitumika kuweka chini ya uangalizi hali ya kisiasa ya Ufaransa. Wanasiasa wanaofadhiliwa na Wamasoni walihamasisha dhana ya Kimasoni, siri zilizojikita za Wamasoni zilifunguliwa kwa wajumbe wa jeshi la Ufaransa, maofisa wa juu na makamanda waliendeshwa kwa kutumia mawazo ya Wamasoni. Wamasoni walifanya kila jitihada kuwatawala wanasiasa na majeshi ya Ufaransa chini ya Umasoni. Ilipofika tarehe 14 Julai 1789, kundi la watu lilivamia jela ya Basteel, Paris. Alama za upinzani uliojikita dhidi ya watawala wa Ufaransa hapo zilidhihirika kwa watu wengi kujitokeza sehemu tofauti nchini Ufaransa.

Huko vijijini na mijini, watu walitoa mawazo yao yaliyojaa chuki dhidi ya utawala wa kifalme. Lakini chuki hizo za Wafaransa hazikuweza kuzimwa moto hadi kufikia mwaka 1793. Mnamo tarehe 21 Januari ya mwaka huo huo, Mfalme Louis XVI alikatwa kichwa mbele ya umati wa watu na kuwa ni sababu ya kufikia kikomo utawala wa Kifalme wa Kifaransa na kusafisha njia ya taifa jengine la Kimasoni barani Ulaya. Kutokana na ufalme huo kuondoka, ilionekana kana kwamba hakuna kitakachowazuia Wamasoni kuitawala Ufaransa kisawasawa. Hata hivyo, kilichotokezea badaye kitawaacha Wamasoni katika kilema kibaya na kitakachotokezea badaye hakika hakikuwa ni kwa mujibu wa mipango ya Kimasoni.

Kijana mmoja kwa jina la Napoleon Bonarparte alikuwa ni askari. Yeye alikosea kidogo kuipeleka Ufaransa kwenye vita vibaya kabisa pamoja na Ulaya pale alipoacha kuufuata muziki wa Kimasoni. Napoleon alijitangaza mwenyewe kwamba yeye ndie Mtawala wa milele wa Ufaransa. Napoleon alilazimishwa kuachana na ufalme huo mnamo mwaka 1814 na alihamishwa kisiwani Corsica. Hata hivyo, mwaka 1815 Napoleon alitokeza kwa mara nyengine tena Paris akihamasisha jeshi jipya likiwa tayari na vita vipya huko Ulaya. Hapo Wamasoni walikuwa na tatizo kubwa mikononi mwao. Uingereza na washirika wake wa Kimasoni hawakuweza kufadhili vita virefu dhidi ya Napoleon bila ya kukaribia kufilisika.

Msaada ulikuja kutoka kwa mtu asiye marufu kabisa. Nathan Rothschild alikuwa ni mkuu akiongoza benki ya kifamilia, lakini kwasababu ya hadhi yao ya Uyahudi, walilazimishwa kufanya kazi kwa kutumia kivuli cha watu wengine. Rothschild alihakikisha kutumia nafasi ya kuwakomboa watu wake na mara nyingi mwenyewe peke yake akidai kurudishwa utambulisho wa Wayahudi kama ni watu walio sawa ndani ya Ulaya, wakiwa nao wana haki ya kufanya biashara wazi wazi. Na kama Wamasoni watazikataa fedha zao mara zote zitaenda kwa Napoleon.

Wamasoni hawakuwa na khiyari isipokuwa kukubali, na biashara ya mkopo ikakamilishwa. Mnamo mwaka 1815 askari wa Kiingereza, Kidachi na Kirusi walikanyaga ardhi ya Waterloo nchini Ubelgiji ambapo walikutana na vikosi vya Napoleon na kuwashinda. Napoleon mara hii alikamatwa na kutorudi tena Ufaransa ambayo hatimaye sasa ilikuwa chini ya muongozo wa Wamasoni. Ingawa wanahistoira wametaja machache katika mahusiano ya Wamasoni ndani ya mapinduzi, Wamasoni wenyewe walilazimika kudhihirisha utambulisho wao wakati wa kipindi hichi muhimu katika historia. Mnamo mwaka 1904 Marc Vadourasamboakiwa ni Mmasoni alitangaza waraka wa makubaliano: "Wamasoni wamefanya (mapinduzi) kwa kujificha lakini kwa namna madhubuti ya kutayarisha mapinduzi, hivyo tupo na makubaliano ya moja kwa moja, Wamasoni wakiwa ndio waanzilishi wa mapinduzi na sifa nilizozipata kutoka kushoto na ambazo nimeridhika nazo zinaonesha kwamba nyinyi waungwana mnakubaliana na mimi kwamba walikuwa ni Wamasoni waliofanya Mapinduzi ya Ufaransa."

Wavumbuzi wa taifa la Marekani walipokanyaga mguu katika jabali la Plymouth, sio tu kwamba walileta watu wasio na haki ya uraia bali pia walileta fikra za Kimasoni za Ulaya. Yale madhila yaliyokimbiwa Ulaya na hao wavumbuzi wa Marekani pia yaliweza kuonekana ndani ya ardhi mpya kwenye mfumo wa utawala wa kibabe wa Kiingereza. Ili kudhibiti na kuendesha katika hali zote taifa hilo jipya la Marekani, Wamasoni walitumia njia zile zile walizotumia kuiteka Ufaransa.

Ingawa ufalme wa Uingereza ulikuwa ukiongozwa na Wamasoni, vita vya Marekani vya kudai uhuru wa Marekani vilihitajika. Na watu walioshiriki ndani ya vita hivyo waligharamika kutimiza ndoto za Wamasoni. Hisia za watu ziliharibiwa katika hamaki na kama zilivyo ghadhabu za Ufaransa zilisababisha vita. Hata hivyo, wakati huu makosa yaliyofanywa huko nyuma hayatarudiwa. Ushindani waliokutana nao Wamasoni dhidi ya Napoleon na jeshi lake huko Ulaya uliwafunza adabu Wamasoni. Kiongozi yeyote wa upinzani anayefuatia ni lazima atekeleze matakwa ya Kimasoni na njia bora ya kufanya hilo ni kuhakikisha kiongozi mwenyewe ni Mmasoni. Na kiongozi aliyepigana dhidi ya Waingereza hakuwa mwengine isipokuwa ni George Washington.

Mnamo tarehe 4 ya Julai mwaka 1776, tamko la uhuru lilitangazwa.
Tarehe 17 Oktoba 1781, hatimaye Waingereza walishindwa na kuyasalimisha makoloni kwa Wamarekani na Taifa la mwanzo la Kimasoni likazaliwa, taifa litakalowakilisha Umasoni katika kila njia. Alama ya kuwepo Umasoni ndani ya Marekani inaonekana wazi kwenye sarafu ya dola ambayo inabeba picha ya raisi wa mwanzo wa Kimasoni George Washington ndani ya ulimwengu, na picha ya alama ya Kimasoni iitwayo "Jicho Moja Linaloona Kila Kitu."

Kumbukumbu zinaonesha kwamba udhibiti na uharibifu wa maoni ya kisiasa ni zana kuu inayotumiwa na Wamasoni katika kushikilia nchi na mataifa. Pale tu watawala na wanasiasa wa nchi wanapodhibitiwa, basi sheria na mfumo wa siasa unaweza mara moja kubadilishwa kwa mujibu wa matakwa yao. Hata hivyo, kuutawala mwili haina maana kwamba umeitawala akili.
Wamasoni wanaelewa kwamba mipango yao ya Serikali Moja inafungamana moja kwa moja na
kuwalainisha watu katika matakwa yao  na hivyo kudhibiti upinzani kutokana na yale wanayoyafanya na tishio kubwa dhidi ya mipango yao ni akili iliyo na fikra huru. Hili kwao ni tishio kubwa kuliko hata jeshi au sheria. Ili kudhibiti tishio hili na kufanikisha malengo yao, Wamasoni wametengeneza mpango wa hatari usiowahi kutengenezwa hapo kabla. Mpango ambao utatawala kila nyanja ya mwanadamu, maisha yako na zana wanazotumia dhidi yako zipo ndani ya nyumba yako mwenyewe, zikikuburudisha wewe pamoja na watoto wako na kidogo kidogo zikikutawala bila ya wewe mwenyewe kulitambua hilo. Ndani ya jamii ya leo, watu wanatumia muda zaidi na zaidi katika vyombo vya kisasa. Luninga, Sinema, Michezo ya Kompyuta, Tovuti, Michezo na vipindi vya ulaghai na Miziki iliyoenea imeganda ndani ya maisha yao.

Na kweli vitu hivi vinasababisha upanuzi wa haraka wa habari ambazo wewe unachukua ndani ya akili yako aidha kwa kutambua ama bila ya kutambua. Habari ndani ya jamii zinaoneshwa katika maadili na tamaduni, tofauti ya zuri na baya hadi namna ya jamii na uchumi unavyotakiwa kutengenezwa. Haya yote yapo mbele ya macho yako katika kila siku ya maisha yako.

Vyombo hivi vya habari, kwa nafasi kubwa vinatumika katika kuweka msingi wa kuamua uoni wa mtu kwa Ulimwengu na kila kitu kilicho mbele yake. Hivyo, kila mtu anapodhibitiwa na vyombo vya habari kama hivi bila ya shaka ataathirika na nguvu za kutawaliwa, na kwa kweli idadi kubwa ya watu duniani inaathirika na fikra zao, na hili hakika ndilo Wamasoni wanaloendelea kuvumbua.

Hakika Wamasoni wanatumia vyombo vya starehe kushurutisha watu katika namna zao za fikra ima wazi wazi au kwa kujificha. Taratibu wanazotumia zinatofautiana lakini lengo lao ni hilo hilo kuingiza imani zao, fikra zao na madhumuni yao kwako wewe katika namna ambayo unaanza kuwafikiria kama ni watu wako. Ushahidi wa kuwepo kwao ndani ya starehe marufu umeenea kila pahala. Ushirikishwaji wa Wamasoni ndani ya uzalishaji huu sio jambo geni. Hail ni miongoni mwa watunzi wa zamani, Wolf Gang Amadeus, Mozart ambaye yeye mwenyewe ni Mmasoni ametengeneza muziki ambao ulikuwa na uonekano wa wazi wa Umasoni. Muziki huo umetungwa kutokana na hadithi iliyochukuliwa kutoka kwa Wamisri wa kale Avysus na Cyrus. Haki za wapagani katika hadithi za kutungwa za kale za Misri za Kabala ni miongoni mwa sifa kuu za Kimasoni. Ni kutokana na asili ya upagani huu wa Kimisri ndio ikapatikana alama ya Shina La Jicho Moja.
Ushahidi wa kuwepo kwa Wamasoni pia unapatikana sana ndani ya miziki marufu ya sasa. Kwa mfano Michael Jackson ambaye anatambulika kama ni mfalme wa pop na anasifika kuwa ni mburudishaji wa wakati huu (wakati huo ilipoandikwa makala hii). Pia anazalisha na kuuza albamu nyingi tu duniani kote, lakini pia anaweza kuunganishwa na Umasoni. Gamba la albamu lake la "Dangerous" lina sifa ya kushangaza kwa kuwa na alama ya Jicho Moja, na pia kuna picha ya mfano wa maji ya mto yanayowaka kwa moto. Inaonesha wazi kwamba yeyote anayeingia ndani ya maji hakika atatumbukia ndani ya moto. Gamba pia lina fumbo ya picha ya mtu mwenye kipara kama ni Alistair Crowley. Yeye mwenyewe alikuwa ni Mmasoni na badaye akawa Mlokole na kuandika kitabu cha "Sheria Mpya Ya Mwanadamu" ambacho kimeeleza ndani yake kwamba siku moja kitachukua nafasi ya Qur-aan kama ni sheria ya mwanadamu.

Ulinganisho huo baina ya Umasoni na fumbo hauishii hapo. Uzalishaji wa miziki inayodhibitiwa na Wamasoni inaingizwa vitendawili vyenye ujumbe wa kishetani. Uchezeshwaji wa kuanza mwisho kuja mwanzo (back tracking) ni njama zinazotumiwa katika kuhifadhi ujumbe ili kuufanya kuwa ni sauti ya muziki katika namna ambayo zinatambuliwa pale tu zinapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo. Pale inapochezeshwa kwenda mbele, msikilizaji hataelewa hata kidogo ujumbe unaochezeshwa.

Ingawa msikilizaji hatakuwa makini kwamba akili yake inakamata ujumbe asiouelewa, lakini katika siku za mbele ujumbe kama huu unaweza kuhifadhiwa ndani ya akili ya mtu na unaweza kuathiri tabia za mtu ama maamuzi yake. Katika namna nyingi, uchezeshwaji wa muziki wa kuanza mwisho kuja mwanzo ni mfumo wa kumfanya mtu atende mambo bila ya kujitambua na ni mfumo wenye kuharibu mara moja. Mfano wa mwanzo wa uchezeshwaji huu ni kutoka kwa msanii wa kike aitwaye Madonna. Unapatikana katika albamu yake marufu kwenye nyimbo ya "Like a Prayer." Hata hivyo, kama utakavyosikia sio mungu anayeonekana kuombwa katika nyimbo hiyo bali ni shetani. Inapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo maneno ya "Ah shetani tuitikie" yanasikika wazi wazi. Pia alama ya Jicho Moja imetumika miongoni mwa video za nyimbo zake Madonna. Ambapo jicho moja linaonekana likitoka katika kichwa chake. Pia anaonekana ndani ya video ambapo amesimama katika maandishi, uchunguzi wa karibu unaonesha kwamba maandishi haya ni ya Kiarabu katika lugha ya Qur-aan.

Mfano mwengine wa uchezeshwaji huu unapatikana katika kundi la "The Eagles" na nyimbo yao inayoitwa "Hotel California". Maneno haya yanapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo yanasikika maneno haya kwa uwazi "Ndio shetani". Na pia hadithi yake wenyewe ni ya kishetani. California ya hapo sio hoteli bali ni mtaa ndani ya Marekani unaoitwa California. Ni katika mtaa huu ambapo makao makuu ya kanisa yalipatikana, lakini sio aina ya kanisa ambalo mtu anaweza kufikiria, bali ni kanisa ambalo baadhi wameliita "Kanisa la shetani." Lililo ongozwa na kuanzishwa na Anthony Sans Delivy, muandishi wa Biblia ya Kishetani. Inaonesha mafundisho ya kanisa hili yamekuwa ndio imani ya watu marufu katika uzalishaji wa bidhaa za starehe kwa waimbaji wote, kuanzia rock hadi main streams, wengine wamefikia hatua ya kushajiisha imani za kanisa hili. Miongoni mwa mjumbe anayetuhumiwa kuhusika na kanisa hili ni mwimbaji wa Rolling Stones anayeitwa Mick Jagger aliyeandika nyimbo ya "Sympathy for the Devil". Inaonesha kwamba kile kilichoanza kama ni Jumuiya ya Wakristo badaye ikabadilika na kuwa ni dini iliyorithiwa hata kwa Wakristo na sasa ina sifa za kishetani zilizochanganywa ndani yake. Ulimwengu wote wa burudani umegandana na ushahidi wa kuwepo kwa Wamasoni wazi wazi au kuzitangaza imani zao kwa fahari kabisa.
(Tanbihi: Mwandishi wa makala hii kutoa mifano ya hiyo miziki, haina maana kuwa miziki inakubalika katika Uislamu, bali ni njia ya kuonyesha upotofu na ushetani wa mielekeo hiyo na inayoambatana nayo. Muziki ni haramu katika Uislamu, na zaidi msomaji asome na asikilize humu:


Hili linadhihirishwa zaidi ndani ya filamu marufu katika big screen au small screen, kwa gharama kubwa za filamu za Hollywood hadi cartoons za kawaida. Wamasoni hawakuacha kuingiza hamasa zao katika kitu chochote ili kushajihisha ujumbe wao wa serikali moja. Matt Growning ambaye ni mtengenezaji wa kipindi cha cartoonmarufu katika historia ya luninga. "The Simpsons" ni cartoon inayotaka uhuru wa madaraka. Matt Growming mwenyewe kwa uwazi kabisa ametangaza kwamba anataka kuziweka fikra zake za kisiasa ndani ya kazi zake. Lakini anataka kufanya hivi katika namna ambayo watu watakubaliana kwa urahisi na mawazo yake. Na njia aliyotumia kulifanya hili ni cartoon ya kitalamu inayoitwa "The Simpsons". Sasa nini haswa hakika Simpsons inatufunza sisi na watoto wetu? Kuna mafunzo mengi (mabaya) yanayofundishwa kwetu, haya yanahusu kutotii utawala aidha ikiwa ni wa mzazi au wa serikali. Tabia mbaya na kutofuata amri ni njia ambazo zinatumika kupata hadhi miongoni mwa watu na kwamba ujahili ni sifa nzuri wakati elimu ni kitu kilichopitwa na wakati. Hata hivyo, kitu kinachotisha haswa ni mambo yaliyojificha chini ndani ya miongoni mwa vipindi vyake.

Kipindi ambacho baba mtu wa familia anayeitwa Homer Simpson anawahamakia kundi linaloitwa stone cutters. Alipojiunga na kundi hilo, wafuasi wenziwe wanatambua alama ya kuzaliwa inayofanya kundi lote kumtangaza kuwa ni aliyechaguliwa lakini kwa hadhi yake na tabia zake yeye Homer Simpson anajidanganya mwenyewe kwa kujidhania kwamba yeye ni mungu. Mtu anaweza kulidharau hilo na kuelewa kwamba jambo hilo ni la cartoon ya kitoto, burudani na kitu kisicho na dhara. Lakini nguvu iliyokuwa nayo kwa watazamaji inafanya kuwa ni njia ya kuathiri watu kwa kuwabadilisha bila ya wenyewe kujitambua. Watengenezaji wake wanakiri kwamba wanaingiza propaganda zao za fikra za kisiasa kwa watazamaji katika njia iliyojificha. Fikra zinazoenezwa kupitia luninga ya nyumbani zinasambaa mbali sana kuliko michezo inayooneshwa sinema. Na ni kupitia vyombo hivi kwamba dhana mpya inawasilishwa. Nayo ni dhana ya kiongozi mmoja kwa ulimwengu mzima.


Inaendelea in  Shaa Allaah…

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only